Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni na Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa wakizindua rasmi promosheni mpya ya Shangwe Shangwena inayoendana na maadhimisho ya miaka 20 ya Vodacom na  msimu huu wa sikukuu ambapo wateja wa M-Pesa watajishindia magari matano aina ya Renault kwid na zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi 3 bilioni.


Mkurugenzi wa M-Pesa , Epimack Mbeteni akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Shangwe Shangwena inayoendana na maadhimisho ya miaka 20 ya Vodacom na  msimu wa sikukuu ambapo wateja wa M-Pesa watajishindia magari tano aina ya Renault kwid mpya na zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi 3 bilioni. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa.



·       Wateja kujishindia zawadi kemkem zenye thamani ya shilingi 3 bilioni katika msimu huu wa sikukuu.

·       Wateja kujishindia magari mapya 5, Pesa taslimu shilingi 1 milioni kwa wateja 25, muda wa maongezi na simu.

Dar es Salaam, 21 Novemba 2020. Mwaka huu Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali, Vodacom Tanzania PLC inasherehekea miaka ishirini ya utoaji huduma tangu ilipoanza kufanya kazi nchini Tanzania. Katika kipindi hiki, kampuni hiyo imeongoza kuleta mabadiliko katika mifumo ya mawasiliano ya simu, mfumo wa malipo, na hivyo kubadilisha maisha ya mamilioni ya Watanzania.

Ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20, Vodacom Tanzania PLC leo imezindua kampeni ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama "Shangwe Shangwena" ambapo kupitia kampeni hii, Vodacom itawazawadia wateja wake ambao wamejikita zaidi katika mtindo wa maisha wa kidijitali kwa kutumia mfumo wa malipo ya kijanja wa M-Pesa.

Wateja hawa zaidi ya 15 milioni, watajishindia zawadi zenye thamani ya Shilingi 3 Bilioni zikiwemo  magari mapya 5, zawadi za pesa taslim, rejesho la fedha pindi mteja anapolipia bidhaa au kutuma hela  kupitia M-Pesa, MB za bure, muda wa maongezi, jumbe fupi (SMS) pamoja  na punguzo la bei pindi mteja anapofanya manunuzi ya simu janja kwa kutumia M-Pesa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC Linda Riwa alisema kwamba anajivunia hatua ambayo Vodacom imefikia katika miaka ishirini iliyopita kwa kukuza maisha ya kidijitali nchini.

"Maono yetu ya kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali kupitia teknolojia sasa yanathibitika, kwani ubunifu wa bidhaa na huduma zetu umeleta matokeo chanya kwenye jamii kwa mfano mfumo wa malipo ya M-Pesa, suluhisho kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kupitia Lipa kwa Simu, mikopo kupitia M-Pawa na Songesha, Vodacom imebadilika kutoka kampuni ya mawasiliano tu na kuwa mwezeshaji wa maendeleo ya kiuchumi katika jamii,” alisema Bi Riwa.

Kampeni ya Shangwe Shangwena itawazawadia wateja zawadi mbalimbali na ofa maalum, zitakazowawezesha kufurahia huduma za mawasiliano wakati huu wa msimu wa sikukuu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni aliwashukuru wateja kwa uaminifu wao kwa miaka 20, na pia kwa kupokea maendeleo ya kiteknolojia na kusema kuwa msimu huu kampuni hyo inataka kusherehekea pamoja na wateja wake kupitia kampeni hii ya Shangwe shangwena.

 “Wateja wanapata nafasi ya kushinda, wakati wowote wanapotumia huduma za M-Pesa kwa kufanya moja au yote kati ya haya; kufanya miamala ya fedha kati ya mtu na mtu (P2P), malipo ya biashara kupitia Lipa kwa Simu, Kuhamisha pesa kutoka Benki kwenda M-Pesa (B2C), Malipo ya huduma kama vile Luku, Dawasco nk, pamoja na ununuzi wa vifurushi, muda wa maongezi na simu janja au vifaa vya simu,” aliongeza Mbeteni.

Mbeteni aliwahimiza wateja kuendelea kutumia huduma tofauti za kidijitali kutoka Vodacom ili wajiongezee nafasi ya kushinda zawadi kemkem na za kufurahisha zinazotolewa wakati wa msimu huu  wa sikukuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...