Picha ni Bw. Daudi Mkoma Mtaalam kutoka katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkoani Ruvuma, akiongea katika mkutano na wakulima wa skimu ya Umwagiliaji ya Nakahuga iliyopo Peramiho wilayani Songea.
baadhi ya wakulima wa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Nakahuga wakifuatilia mkutano na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mkulima katika skimu ya kilimo cha uwagiliaji ya Nakahuga iliyopo Peramiho wilayani Songea Bw. Albert Mtani akiuliza swali wakati wa mkutano na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Na Mwandishiwetu – Peramiho

Wakulima katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Nakahuga iliyopo Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma wameipokea sheria ya Taifa ya kilimo cha umwagiliaji na kuonesha utayari wa kuchangia katika mfuko wa maendeleo yakilimo cha umwagiliaji kwa kukiri kuilewa sheria hiyo mara baada ya mafunzo waliyopata  toka kwa wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

 Akizungumza wakati wa mkutano wa majumuisho uliofanyika katika kijiji cha Nakahuga,mmoja wa wakulima hao Bw. Albert Mtani  alisema kuwa kilimo cha umwagiliaji kwao ni mkombozi kwani ni kilimo cha uhakika.

 “Binafsi ninaishukuru serikali kwa kuleta mradi huu nani naamini inania njema ya kuendelea kuboresha miondombinu katika skimu hii na kwa kuwa tunapata faida nyingi zitokanazo na shughuli zetu zakilimo, hivyo sio ni tatizo kwenye uchangiaji katika mfuko kwani ninaamini kuwa mifereji itakapo haribika kwa namna yoyote ile serikali itaitengeneza kupitia mfuko huo,  na tutaendelea na shughuli zetu za kilimo bila wasiwasi.” Alisema.

Sambambana hilo kwa nyakati tofauti katika ushiriki wa mkutano huo, baadhiya wakulima walisikika wakisema kuwa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji sasa imekaa vizuri kwani kabla yakuwepo kwa sheria hiyo ushirikishwaji wa wakulima kuhusu shughuli za umwagiliaji ulikuwa ni mdogo na kulikuwa na usimamizi mbovu wa miundombinu yaumwagiliaji

Waliongeza kwa kusema kuwa sheria ya  Taifa ya umwagiliaji pia itaweza kusaidia kutatua migogoro midogo midogo iliyopo katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...