Na.Khadija seif, Michuzi tv

TAKRIBANI washiriki 20 wa Mashindano la Miss Tanzania waingia rasmi kambini.

Akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ambayo imepewa dhamana ya kuandaa Mashindano hayo (The look company) Basilla Mwanukuzi amesema warembo hao wapatao 20 tayari wameingia kambini.

"Mchakato wa kupata washiriki ulifunguliwa rasmi March 2020 na tulianza usahili kwa Kanda ya Kati."

Mwanukuzi ameeleza jinsi gonjwa la covid 19 ( Corona) na gonjwa la Corona wakati tunaenda kufanya usahili Kanda ya kaskazini.

"Kutokana na shida hiyo tulilazimika kuhamishia usahili kupitia online na kupata takribani washiriki 100 wenye vigezo,tuliwachuja warembo 50 na hatimae tukatapa warembo 20 ambao wameingia kambini rasmi."

Aidha ametaja Kanda ambazo zilijumuishwa katika mchakato wa kupatikana washiriki hao ni pamoja na Kanda ya ziwa,Kanda ya juu kusini,Kanda ya kati pamoja na Dar es salaam.

Pia amefafanua kuwa kwa mwaka huu kitu cha tofauti kwa warembo hao ni wameshaanza kuandaa mpango mkakati (project ) mapema kwa ajili ya kusaidia jamii inayowazunguka.

"Mara nyingi wamekua wakifanya mipango mikakati hii pale anapopatikana mshindi tayari lakini kwa mwaka huu imekua tofauti na kuwapa fursa washiriki wote kuonyesha uwezo wao na dhamira zao katika kusaidia jamii sambamba na kuwepo kwa kipengele cha kuulizwa maswali magumu wakiwa kambini ili kuwajengea uwezo wa kujieleza kwa ufasaha mbele ya jukwaa."

Muandaaji huyo ametaja zawadi kwa mshindi atakaepatika ni gari aina ya Subaru pamoja na washiriki wengine watapata fedha,viatu pamoja na kitanda kutoka kwa wadhamini sanjari na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu spika wa bunge Tulia ackson na Mashindano hayo yatafanyika desemba 5 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.

Huku Moja ya mdhamini wa shindano hilo Amina swedi kutoka Kampuni ya (it's all about cards) ambayo inajihusisha na kutengeneza kadi za shughuli mbalimbali akitoa ya moyoni kutokana na kuendelea kudhamini shindano hilo kwa Mara ya 3 mfululizo.

"Tangu mashindano haya yamepokelewa na Mwanamke wa nguvu Basilla Mwanukuzi tumeona ipo haja ya kuendelea kumpa ushirikiano ndio maana tumeamua kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo mataji ya warembo wetu."

Hata hivyo amina ameongeza kuwa mwaka huu anategemea kuona Mshindi ambae ni Mrembo sana na atatuwakilisha vizuri mashindano ya dunia (Miss world).Mkurugenzi wa Kampuni ya The look Basilla Mwanukuzi akiambatana na Mshindi wa Shindalo Miss Tanzania 2019, Sylivia Sebastian pamoja na wadhamini mbalimbali akizungumza na waandishi wahabari katika ukumbi wa serene   jijini Dar es salaam wakati akitangaza rasmi jumla ya washiriki 20 wa Shindano la Miss Tanzania kuingia kambini.

Mmiliki wa Kampuni inatongeneza kadi pamoja na mataji ya warembo hao Amina swedi akizungumza na waandishi wahabari jinsi walivojipanga kwa mwaka wa 3 wakiwa Kama wadhamini wa Shindalo hilo.
Warembo 20 ambao wameingia kambi ya Shindano la Miss Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...