Na Amiri Kilagalila,Njombe

Serikali wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe imesema ipo mbioni kutengeneza utaratibu wa kuwabana na kuwachukulia hatua kali za kisheria vijana wanaojiunga na mafunzo ya jeshi la akiba na kisha kushindwa kumaliza mafunzo hayo kwa kutoroka ili hali tayari wameshafahamu mbinu za awali za kijeshi.

Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Lauteri Kanoni ameyasema hayo mbele ya hadhara ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba 166 wakiwemo wanawake 21 waliomaliza mafunzo kwenye Kata ya Makoga wilayani Wanging’ombe mkoani humo ambapo amewaasa wahitimu kuwa wazalendo na nchi yao..

“Tutatengeneza utaratibu ukishajiandikisha na ukishahudhuria mafunzo,ukapata ABCD za jeshi kidogo harafu ukatoroka tutakukamata kama muarifu.Kwasababu tayari umepata siri za jeshi na sasa hivi mnatambulika kama askari na kupitia kiapo chenu mmeapa kwamba mtailinda na kuitumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa”alisema Lauteri Kanoni

Nao wahitimu wa mafunzo hayo akiwemo Josmo Mlwanda wamesema katika mafunzo hayo wamekumbana na changamoto ikiwemo ikiwemo vijana kuto tambua umuhimu wa mafunzo ya mgambo pamoja na upotoshaji kuwa mafunzo hayo ni unyanyasaji

Aidha suala la uhaba wa Sare za jeshi la akiba maarufu mgambo nalo limeonekana ni changamoto kubwa ambapo mshauri wa mgambo wilayani Wanging’ombe, Kaptein Godwin Kimaro amesema baadhi ya wanafunzi wameshindwa kumudu ghalama za mavazi huku mkuu wa wilaya hiyo akiagiza halmashauri kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya kununua mavazi hayo.

“Naielekeza halmashauri kutenga bajeti kwa kila mwaka kwa ajili ya kununua mavazi ya askari mgambo”aliagiza Kanoni.

Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Lauteri Kanoni wakati akizungumza mara baada ya kukagua jeshi la akiba katika kata ya Mkoga.
Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Lauteri Kanoni akikagua gwaride la jeshi la akiba (mgambo)
Jeshi la akiba wakionyesha umahili wa kutumia silaha wakati wa mahafali.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...