Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ametangaza kuwa kutokana na urithi mkubwa wa sanaa uliopo nchini ikiwemo muziki, filamu, ngoma na uga mwingine, sekta hiyo inapaswa kuhakikisha inaiburudisha jamii yetu ya wachapakazi ipasavyo na kwa kuanzia Serikali kwa kushirikiana na wadau itaratibu Tamasha kubwa la aina yake la Muziki na Sanaa litakalotumia jina la moja ya vivutio vikubwa vya utalii hapa nchini. Adha, amesema kuanzia mwakani Serikali pia itashirikiana na wadau kurejesha tuzo za muziki na sekta nyingine za Wizara hiyo.

"Moja ya kazi kubwa ya sekta ya sanaa nchini ni kuhakikisha jamii yetu inayochapa kazi sana kwa sasa inaburudika ipasavyo, sasa naona sanaa inakuja tu pale panapokuwepo mdhamini au mwandaaji fulani asipokuwepo hakuna matukio na nchi iko kimya. 

Serikali sasa inakwenda kuchechemsha sekta hii kwa kuratibu Tamasha kubwa sana litaanzia Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kuendelea kuungana na Tamasha la Kimataifa la Sanaa Bagamoyo. Tusisibiri wadhamini, wakija sawa, kama wako likizo, basi mimi nasema sisi wenyewe tunaweza kwa umoja wetu sasa tukutane Uwanja wa Uhuru Disemba 26 mwaka huu na kisha Desemba 27 twende Bagamoyo.

"Wasanii wakoungana watajaza Uwanja. Twende Tutateremsha wasanii wetu wote ambao ni urithi wa sasa na baadaye wa nchi hii halafu tuone kama watu hawatakuja," alisema Dkt. Abbasi akiwa katika siku ya tatu ya kukutana na wadau wa sanaa kwa kukutana na wasanii wa Bongo Movie.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...