TUKIWA kwenye janga la Corona, linalosababisha waathirika wapatao 500,000 na vifo 8,000 kila siku ulimwenguni, shirika la kidini lenye makao yake Korea kusini, liitwalo Shincheonji Church of Jesus, hekalu ya hema ya ushuhuda (lijulikanalo kama kanisa la Shincheonji) liliandaa mkutano wa maombi kwa njia ya mtandaoni “ikiwa ni mara ya tatu kufanyika kwa mkutano huu wa maombi” mnamo tarehe 15 Novemba.

Tukio lilirushwa mubashara kupitia akaunti ya Youtube ya kanisa la Shincheonji, mkutano huu wa maombi haukuandaliwa kuombea wahanga wa corona na familia zao tu bali pia serikali, wahudumu wa afya na wote wanaojitolea katika mapambano dhidi ya COVID-19. Wakiwa pamoja na waumini  wa kanisa la shncheonji 200,000 wa ndani na nje ya korea kusini, watu wapatao 56,000 duniani kote wenye dhamira ya kukomesha janga hili waliungana kwenye maombi kwa wakati huo.

Viongozi wa kidini kutoka ulimwenguni kote waliongeza matamanio yao ya kukomesha COVID-19 kwenye mkutano huo wa maombi. Maneno yao yalibeba uzito na uwazi walipofanya kazi na Mwenyekiti Man Hee Lee, ambaye ni mwakilishi wa HWPL, shirika la amani la kimataifa lisilo la kiserikali.

Mwenyekiti Lee, kama veterani wa vita ameshashiriki shughuli nyingi za amani zinazolenga pendo la ubinaadamu kwa waathirika wa vita na maneno ya Yesu ‘utukufu mbinguni na amani duniani,’’ akiwa kama muumini. Alipendekeza mkutano wa maombi kwa  njia ya mtandaoni kwa sababu ‘ ulimwengu unateseka na corona=COVID-19, watu wenye dini ulimwenguni inawapasa kuomba kwa pamoja kukomesha janga hili’’

“Watu wengi wanateseka kutokana na janga hili la Corona.Katika kanisa letu watu wengi waliathirika hasa mapema mwezi Februari. Waumini na wananchi wote kwa pamoja waliteseka sana. Lazima tusonge mbele na tumuombe Mungu kwa ajili ya kukomeshwa kwa janga hili ulimwenguni, kwa ajili ya taifa na watu,”alisema

Viongozi wa dini 352 wa Ubuddha, Usikhi, Uislam na Uhindu, wakiwakilisha nchi 73 walishiriki kwa moyo mmoja kwenye mkutano huo wa maombi bila  kujali dini au madhehebu. Walikuwa na kusudio  moja la hitaji la kulishinda janga wakiwa mstari wa mbele kama viongozi wa kidini.

Dkt. AnakAgungDiatmika, katibu wa International Relationship of PHDI Jarkata alisema,’Kwa kweli kutoka ndani ya mioyo yetu tuzingatie kuwa SISI NI WAMOJA. Yatupasa tuendelee na maombi mpaka mwisho wa janga la COVID-19 katika dunia yetu na tuendelee kuunganisha nguvu kama viongozi wa kidini katika kuitunza amani ya dunia,maelewano,haki na ustawi. Nina fuaha sanakuungana katika hili, hakika linaleta amani ya dunia na maelewano.’’

Baada ya mkutano huu wa maombi, wagonjwa waliopona COVID-19 wapatao 4,000 ambao pia ni waumini wa kanisa la Shincheonji watajitolea utegili(blood plasma)  kwa ajili ya kutengenzea matibabu kupitia utegili inayopatikana kwa mtu aliyepona corona. Kanisa la Shincheonji limejitolea mara mbili utegili kutoka waumini 1,700 mapema mwezi Julai na Septemba na kati yao, waumini 312 waliopona walichangia mara mbili.

Kutokana na uchangiaji huo mkubwa wa utegili, Rt.Mh. HrantBagratyan, waziri mkuu mstaafu wa Armenia, ametuma salamu zake za pongezi zenye ujumbe, ‘suala la hawa walioamua kujitolea utegili(blood plasma) kwa ombi la serikali ni la kupongezwa. Kama chanjo inatengezwa kupitia utegili basi itasaidia dunia nzima.’’

Afisa wa kanisa la Shincheonji alisema ‘Tunafanya ibada za mtandaoni tangu tarehe 18 Februari na tunaomba kila mwisho wa ibada kwa ajili ya kukomeshwa kwa COVID-19, usalama wa mamlaka za karantini na wahudumu wa afya na kupona kwa wagonjwa. Tutafanya kila liwezekanalo tukijitwika majukumu mpaka pale janga la COVID-19 litakapokwisha.’’


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...