Na Piason Kayanda, Michuzi TV

TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeshindwa kufua dafu katika mchezo wa Fainali ya Michuano ya CECAFA U20 baada ya kupokea kichapo cha bao 4-1 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Uganda U20.

Katika mchezo huo wa Fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Black Rhino Academy Karatu, mabao ya Uganda yalifungwa na Richard Basangwa dakika ya 12, Steven Sserwadda dakika ya 44, Ivan Bogere dakika ya 62 na Kenneth Semakule dakika ya 72.

Bao pekee la Ngorongoro Heroes limefungwa na Mshambuliaji Abdul Kassim kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 30.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelo amesema Wachezaji wake wamefungwa kutokana na timu hiyo kuona tayari wamefuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya miaka 20 (AFCON U20,) Amesema ameshukuru kufika malengo hayo.

Ngorongoro Heroes na Uganda zote zimefuzu Michuano ya AFCON U20, Michuano itakayofanyika nchini Mauritania mwakani 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...