Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka wananchi wa
Mkoa huo kuhakikisha kila Jumamos wanafanya zoezi la usafi wa mazingira
kuanzia saa 12 Asubuhi hadi saa tatu ili kujikinga na magonjwa ya
Mlipuko na kuliweka jiji kuwa Safi.
RC Kunenge ametoa maelekezo
hayo wakati alipokuwa anazungumzia zoezi la usafi linalotaraji kufanyika
Jumamosi ya Disemba 05 ambapo amesema Mkoa umejipanga vizuri
kuhakikisha magari ya kubeba taka yanakuwa ya kutosha kwenye kila
maeneo.
Aidha RC Kunenge amewaelekeza Wakuu wa Wilaya za Jiji
hilo kuhakikisha wanasimamia usafi Katika maeneo yao na kuhakikisha
suala la usafi linazingatiwa na kila mmoja.
Pamoja na hayo RC
Kunenge ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuhakikisha suala la usafi
linakuwa sehemu ya maisha yao na sio kusubiri kushurutishwa na Sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...