Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Hamis Taletale akizungumza na wananchi wa kata ya Ngerengere wakati akitimiza ahadi yake ya ukarabati wa barabara hiyo ambayo haikuwahi kupata matengenezo kwa takribani miaka 15 Sasa, leo jimboni humo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC,) ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Habari, Elimu  na Mawasiliano Jamila Mbarouk akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo ambapo amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kusimamia miradi ya namna hiyo, na kuwataka watanzania kuwa walinzi na wazalendo katika miundombinu ya reli, leo Morogoro Kusini Mashariki.
Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Morogoro Bakari Msolwa akizungumza na wananchi  kuhusiana na utekelezaji wa miradi jimboni humo na kueleza kuwa kasi ya Mbunge Taletale ni kubwa na maendeleo yatafikiwa kwa urahisi zaidi, leo Morogoro Kusini Mashariki.
Mwakilishi wa Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Gebo Mlangwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ukarabati wa barabara hiyo na kueleza kuwa wamekarabati kilomita 10 kwa fedha za Serikali kupitia programu ya mfuko wa maendeleo na amemshukuru Mbunge Taletale kwa kutafuta wadau ili waweze kusaidia kutimiza malengo, leo Morogoro Kusini Mashariki.
Kazi ikiendelea.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

*TRC yawaomba wananchi kulinda miundombinu ya reli

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) kwa kushirikiana na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamis Taletale maarufu kama 'Babu Tale' wameanza mchakato wa kukarabati barabara ya Ngerengere iliyokuwa kero kwa wananchi kwa zaidi zaidi ya miaka 15.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC,) Mkuu wa kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa TRC Jamila Mbarouk amesema, TRC kwa kushirikiana na mkandarasi anayejenga reli ya kisasa wameshiriki kwa kutoa msaada huo kwa jamii baada ya Mbunge Taletale kuwafuata na kuwaeleza changamoto zinazowakabili wananchi wa Morogoro Kusini Mashariki.

"Tunaelewa kuwa reli ya kisasa inajengwa kwa kodi za watanzania na mradi huu lazima itunzwe na kuthaminiwa na wana Ngerengere na Watanzania kwa ujumla, na tutaendelea kushiriki katika kusaidia jamii kama Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli inavyosimamia katika kuhakikisha mtanzania anavyofanya shughuli zake kwa amani... Wana Ngerengere mmepitiwa na mradi huu wa reli ya kisasa niwahakikishie mapema mwakani mtakuwa wa kwanza kunufaika na mradi huu" Amesema.

Amesema, TRC kwa kushirikiana na Yepi Merkezi itachonga na kushindilia barabara hiyo kwa kilomita 60.54  zilizobaki na wataendelea kutekeleza na kushiriki katika miradi hiyo kwa jamii kama walivyoaminiwa na Serikali.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Hamis Taletale amesema, ukarabati wa barabara hiyo katika tarafa ya Ngerengere ni moja ya ahadi aliyoihaidi jimboni humo.

"Katika kampeni zangu nilihaidi kukarabati barabara hii, niliwahaidi wana Ngerengere hawatopanda malori tena nimeanza kazi katika barabara hii ambayo haijawahi kupitiwa na katapila kwa miaka 15 na tutafanya mengi zaidi katika Jimbo hili." Amesema.

Mbunge Taletale amesema atafanya kazi kwa spidi katika kuboresha sekta za Mawasiliano, afya na elimu kama Serikali ya awamu ya tano ilivyodhamiria.

"Huu ni mwanzo tuu nitatembea kwa speed katika kuilinda ilani ya Chama cha Mapinduzi, na tutaendelea kushirikiana na wakazi wa Ngerengere katika kuyafikia Maendeleo...Na ndani ya miaka hii mitano nitahakikisha ninajenga ofisi ya chama kwa kila kata ikiwa ni pamoja na usafiri." Amesema.

Kuhusiana na suala la elimu, Mbunge huyo amesema kuwa ameshawashirikisha wadau wa sanaa hasa wasanii wakiwemo Diamond Platnumz, Ali Kiba, Rayvanny na Mbosso ambao watachangia madawati ili wananfunzi waweze kusoma vizuri na kusema kuwa kero ya mtando katika eneo la Ngerengere litakoma ndani ya miezi mitatu ijayo.

Akimwakilisha Meneja TARURA wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Gebo Mlangwa amesema, barabara hiyo ni moja ya barabara 84 za Wilaya hiyo na katika tarafa ya Ngerengere tayari wamekarabati kilomita 10 kwa kiwango cha changarawe kwa gharama ya shilingi milioni 200 fedha za maendeleo zilizotolewa na Serikali.

Amesema, TRC wameanza kazi hiyo waliyohaidi jana na tayari wamechonga kilomita 3 na watachukua wiki tatu kukamilisha barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...