Na Mwandishi wetu Globu ya Jamii
IKIWA ni miaka 28 sasa tangu kuanzishwa kwa maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Desemba 3, 2020 watu wenye ulemavu nchini Tanzania bado walia na miundombinu rafiki ya vyoo kwa watu wenye ulemavu.

Ili kuhakikisha watu wenye walemavu wanapata haki sawa kama watu, Mwanzilishi wa Taasisi ya Keep Life, Sophia Mbeyela amehamasisha jamii kujenga Vyoo rafiki kwa watu wenye ulemavu nchini hasa mashuleni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 5, 2020, amesema kuwa katika kudhimisha siku ya watu wenye ulemavu dunia ambayo hufanyika kila mwaka Desemba 3, kwa mwaka huu wamejikita katika kuhamasisha ujenzi wa vyoo rafiki hasa mashuleni kwaajili ya wanafunzi walemavu wanaopata huduma ya elimu hapa nchini.

"Kwa sababu sasa hivi jamii kubwa imeelimika kupeleka watoto wenye ulemavu mashule kwahiyo tunaomba serikali na jamii nzima tuungane pamoja katika kuhakikisha upatikanaji wa vyoo rafiki mashuleni vinapatikana." Amesema Sophia.

Hata hivyo Sophia amewahamasisha walemavu wajikite katika kupambana kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa Taifa kwa Ujumla.

Akizungumzia hali ya sasa na ya kipindi cha nyuma cha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu Sophia amesema kuwa angalau haki zimeanza kutekelezwa japo kiwa sio kwa asilimia 100.

"Kwahiyo sisi kama wadau wa watu wenye ulemavu tunaihamasisha jamii, serikali na wadau wote tuendelee kupambana ili kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zote zinatekelezwa kama haki za watu wengine."

Hata hivyo Sophia ametoa wito kwa jamii kiwatambua watu wenye ulemavu popote pale walipo na kuhakikisha wanapata fursa sawa hasa Elimu ya Afya ya Uzazi, elimu ya Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watu wenye ulemavu.

Pia kuhakikisha jamii inawajumuisha walemavu kwa vitendo kupata elimu na stahiki zote zinazojitokeza katika jamii.

Kwa upande wake, Mzazi mwenye mtoto mwenye ulemavu, Agnes Mbeyela ameomba viongozi wa serikali kuanzia serikali ya mtaa mpaka serikali kuu kuwaingiza wazazi wa watoto wenye ulemavu katika Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF)..

"Familia za watoto wenye ulemavu wanahangaika sana hadi imefikia kipindi wanawaweka watoto barabarani ili wapate chochote, kwahiyo wawaingize kwenye kaya masikini nawaomba serikali." Amesema Agnes


Mwanzilishi wa Taasisi ya Keep Life, Sophia Mbeyela akiongoza katika maandamano ikiwa ni moja ya kusheherekea siku ya walemavu duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Desemba 3. Maandamano hayo yamianzia Kituo cha polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam hadi Kituo cha Donibosco.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Keep Life, Sophia Mbeyela 

Mwanzilishi wa Taasisi ya Keep Life, Sophia Mbeyela  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya maandamano kwaajili ya kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...