MAHAKAMA ya Wilaya ya Iringa, imewahukumu watu watatu, Richard Mbundamila, Taford Kalinga na Haruni Mgawo, kutumikia kifungo cha miaka 44  jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha, kutoroka chini ya Ulinzi na Kujeruhi.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha na miaka saba kwa kila kosa kwa makosa ya Kujeruhi na kutoroka chini ya Ulinzi.

Hukumu hiyo imesomwa leo Desemba Mosi,2020 na Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa Liad Shamshana.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shamshana amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake na vielele, wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa walitenda kosa.

Hata hivyo mahakama imesema kuwa adhabu zote nitaenda kwa pamoja hivyo washtakiwa watakaa gerezani miaka 30.

Katika kosa hilo upande wa Mashtaka uliwasilisha vidhibiti kadhaa vikiwemo bunduki aina ya uzi guni, mashoka Saba, Mapanga matano,risasi mbili, maganda mawili ya risasi pamoja na sare tatu za wafungwa.

Mapema ilielezwa mahakamani hapo kuwa, watuhumiwa hao walikuwa wafungwa waliokuwa wakitumikia vifungo mbalimbali ambapo siku ya tukio walienda kutafuta kuni na wakiwa huko walimvamia askari aliyekuwa anawalinda na kumkata panga kichwani kisha kumnyang'anya bunduki na kuondoka nayo.

Katika tukio hilo mtuhumiwa mmoja aliuawa katika mapambano akiwa huko Njombe ambapo silaha iliyoibiwa ilikombolewa.

  Mawakili wa Serikalii walioendesha kesi hiyo ni Edna Mwangulumba na Brandina Manyanda.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...