Katibu Mkuu wa  Wizara  ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akisistiza jambo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo 
Katibu  Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo anayefuatia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
MBUNGE  wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwijuma alimaarufu "Mwana FA" kushoto akimueleza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga  ukubwa wa tatizo la maji wilayani Muheza wakati wa ziara yake
MKUU  wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara  hiyo wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga na kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
MENEJA wa Ruwasa wilaya ya Muheza akieleza jambo wakati wa ziara hiyo
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kulia akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na kushoto ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
Mkurugenzi  wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara yake wilayani Muheza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwijuma alimaarufu Mwana FA

WIZARA ya Maji imehaidi kupelekea fedha wilayani Muheza Mkoani Tanga ili mradi wa kutoa maji eneo la Pongwe wilayani Tanga hadi Kitisa wilayani Muheza ulioishia njiani uweze kusambaa kwa wananchi ili kupunguza changamoto ya tatizo la maji wilayani humo.

Hayo  yalisemwa na Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo ambapo alisema fedha hizo ambazo makadirio yake ni Bilioni 4 watazipeleka kidogo kidogo mpaka  zitakapokamilika

Alisema  ni kweli fedha hizo ni nyingi lakini hawawezi kuzipata kwa mkupuo watakuwa wakipeleka kwa awamu wanaweza kutumia na kuangalia wapi wamebakiza na maelezo yake ni kwamba mradi mkubwa wa kutoa Maji Mto Pangani utakapoanza uungane na mradi ambao unaendelea.

"Niwahakikishie  wananchi wa Muheza wizara ya maji haitakuwa kikwazo kuwapatia huduma ya  maji najua tumechelewa hivyo mwezi Desemba tutawaletea fedha mfanye manunuzi ya mabomba na kabla ya mwezi huu haujaisha tuone mmeanza kuchimba mitaro na kulaza mabomba naliongea hili kwa sababu Rais Dkt John Magufuli alihakidi kwenye kampeni anataka wananchi wapate maji”Alisema

Aidha  alieleza pia  Rais Dkt John Magufuli alisema na serikali anayoiongoza haitavumilia kuona wananchi wanakosa maji na aliwalenga wananchi wanyonge hivyo raisi ametoa fedha kupitia mfuko wa maji na wanaangali maeneo  yeye shida ya maji na wanapeleka na kueleza mradi wa maji wa Mto  Pangani upo njiani.

“Lakini  niwahaidi kwamba wizara ya maji haitakuwa kikwazo kwenye suala la maji wilaya muheza nimepitia ripoti kwa kweli hazipo vizuri kwenye wilaya ya Muheza na Mkinga kuna changamoto kubwa ya maji nimetoa maelekezo bahati nzuri wataalamu wa wizara ya maji wamekwisha kuingia wataanza kushughulika na Mkinga”Alisema

Alisema  kwa bahati nzuri wilaya ya Muheza walikwisha kufanya kazi nzuri ya kutoa maji Pongwe mpaka Kitisa na yamesogea kilomita sita kuna bomba halijaakaa vizuri nalifahamu hilo ila kuna mradi mkubwa wa Mto Pangani lakini hatuwezi kusubiri mradi huo.

“Nafahamu  kuna mradi mkubwa wa Mto Pangani lakini hatuwezi kusubiri mradi huo kama maji ya Tanga yanaweza kufika hapa na bahati nzuri Muheza tumeikabidhi Tanga Uwasa na nimekwisha kuwaeleza leo kwamba lazima huduma ya maji Muheza ifanane na Tanga mjini na Pangani kwa hiyo watashughulikia”Alisema

Awali  akizungumza wakati wa ziara, Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma almaarufu Mwana FA alisema maji ndio tatizo kubwa kwenye Jimbo hilo na nililiahidi wakati wa kampeni na hata Rais alipotembelea mkoa wa  Tanga tukiwa Korogwe nililihubiri suala hili.

Mbunge  huyo alisema pamoja na kwamba serikali ya Rais Dkt John Magufuli inafanya kazi nyingi nzuri lakini hili la maji linawaweka kwenye wakati mgumu na watu hivyo wao wakamuomba tena mradi uliokuwa unatoa maji Pongwe Kilapura ambao ulikuwa na Tanki la lita laki saba ulikuwa umekwisha kuingiza maji NHC kwenye matanki.

Alisema  lakini tatizo likawa kwenye mfumo wa usambazaji na kukawa na maeneo kwamba utafanayiwa kazi  na hata Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alipokuja na kutoa namba zake akawa mdomo wazi kwamba kiasi cha fedha kinachoitajika ni bilioni 4 kwa hiyo mradi wa Bilioni 6.1 bado unahitaji bilioni 4 karibu asilimia 40 mradi haujakamilika.

“Ombi  langu kwao toeni fedha kwenye mfuko wa maji japokuwa wazo la awali lilikuwa kusubiri mradi wa kutoa maji Mto Pangani utakaoanza mapema mwakani ingawa utachukua muda mpaka kukamilika na kufika kwa wananchi”Alisema Mbunge huyo.

Mbunge  Hamisi alisema wanawashukuru wizara hiyo kwa kusikiliza ombi lake hivyo  wanaomba huo mfumo wa utengenezwe kwa fedha kutoka mfuko wa maji halafu mradi wa kutoa maji Pangani utakapofika watoe kiasi kilichokuwa  kimewekwa kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa usambazaji  kiasi cha bilioni 4.

“Kama  fedha zinarudi huko kwenye mradi mwengine zirudishwe huko lakini mfuko wa maji uwasaidie kwa sababu wananchi wanateseka niishukuru serikali ya awamu ya tano kuna sehemu maji yanatoka mara mbili kwa wiki na mara moja  kwa wiki masaa manne”Alisema

Hata  hivyo alisema pia kuna mahali maji yakitoka mara mbili kwa wiki unapigiwa simu tatizo hilo ni deni kubwa kwake na serikali ya awamu ya tano hivyo wanaomba lipatiwa ufumbuzi ili wananchi waweze kuondokana na adha hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...