Na Karama Kenyunko -Michuzi Blog

WATU 64 waliokuwa wamezamia nchini Afrika Kusini wametiwa hatiani mbele ya Mahakimu wawili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na wamehukumiwa kulipa faini ya sh.400,000 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani.

Watuhumiwa hao wametiwa hatiani kwa kosa la kutoka nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na kubali.

Hukumu hiyo imesomwa leo Januari 25, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mbando baada ya washtakiwa hao kukiri shitaka linalowakabili.

Akisoma hukumu kwa washtakiwa 32 kati yao, Hakimu Shaidi amesema, kosa la kutoka nje ya nchi bila kibali sheria imeeleza wazi adhabu yake ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja gerezani na faini isiyopungua laki tatu au vyote kwa pamoja.

"Hakuna familia ambayo iko tayari kumlisha mtu bure hivyo  mnahitaji maandalizi ya kwenda mtaani kupambana na maisha, pamoja na maelezo yenu kuomba mpunguziwe adhabu, Mahakama imewatia hatiani na mnahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Shilingi  laki tano," amesema Hakimu Shaidi.

Kwa upande wake hHakimu Mmbando amewahukumu washitakiwa wengine 32, kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Shilingi 300,000 kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutoka nje ya nchi bila kibali.

Mapema kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili Shija Sitta amedai kuwa, washtakiwa hao  wamekiri wenyewe kutenda kosa na kuisababishia Serikali hasara katika kuwarudisha  nchini ni vyema mahakama iwape adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Washtakiwa hao wanadaiwa, Januari 22,2021 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere ulioko Ilala Jijijini Dar es Salaam,washitakiwa hao wakiwa ni raia wa Tanzania walikutwa uwanjani hapo wakirejea kutoka Afrika ya Kusini bila kuwa na kibali.

"Januari 22, walipelekwa katika ofisi za Uhamiaji zilizopo Kurasini Jijini Dsm  ambapo walichukuliwa maelezo ya awali na kabla ya  kufikishwa Mahakamani kujibu shitaka lililoko mbele yao.

Miongoni mwa washitakiwa hao ni Frank Martine, Abdullah Kujali, Feisal Mnakoma, Ally Bashuti, Ally Mputo, Mtoro Mohamed, Omar Mpoki, Hussein Mnywmani, na Ally Zuh

Wengine ni Martin Mwerela,Limbinda Kapondo,Andrew Makule, Ramadhan Mtopela,Shukuru Totoro,Saray Both na Jabir Sobo.

Hata hivyo baadhi ya washtakiwa wamefanikiwa kukwepa kufung baada ya kufanikiwa kulipa faini na wengine kwenda jela kufuatia ndugu zao kutokuwepo Mahakamani hapo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...