Na Mwaandishi Wetu Mtwara

BANK ya NMB Mkoani Mtwara imetoa msaada vitu mbalimbali vikiwemo chakula kwa waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo ilinyesha siku mbili mfululizo mkoani mtwara.

Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni tano ulitolewa katika vituo vya kuhifadhi waathirika vya Sino na Rahaleo  kwa mda huku serikali ikiendelea kufanya utaratibu wa kuondoa maji katika makazi yao ili waweze kurejea.

Akizungumza wakati anakabidhi msaada huo Meneja wa Huduma Bank ya NMB kanda ya Kusini Mohammed Fundi amesema wameamua kutoa msaada huo ili kuwasaidia waathirika hao ambao pia kuna watoto wadogo pamoja na wanafunzi.

“Tumeamua kutumia kile kiasi tulichanacho kuwasaidia ndugu zetu,. Tumewaletea magodoro, mashuka, unga, sukari, mafuta ya kupikia, mchele, sabuni, chumvi, na mahitaji mengine ili viwasaidie kwa mda huo ambapo wanasubiria utaratibu mwingine,” amesema.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Afisa mtendaji Kata ya Ufukuno Wilaya ya Mtwara Filomena Mgwale ameishukuru benki hiyo ya NMB na kusema kwamba msaada huo ni muhimu sana na utawasaidia waathiriwa hao haswa watoto na wanafunzi ambao kwa sasa wamepoteza makazi yao.

Akizungumzia waathirika waliohifadhiwa Sino, Afisa Kata huyo amesema kuna waathirika kutoka kata ya ufukuni na magomeni wapata 48  huku 15 kati yao wakiwa hawana makazi yao kabisa baada ya kubolewa na mvua na wengine nyumba zao zikiwa zimebolewa upanda na nyingine kuingiwa na maji.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Masumbuku Mtesigwa amesema kuna wahanga wa mafuriko zaid ya 140 ambao wamehifadhiwa katika vituo vitano katika manispaa ya Mtwara Mikindani.

Amesema serikali inafanya jitihada za kuokoa nyumba za wahanga hao ili waweze kurejea kwenye makazi yao na kuendelea na shughuli za maendeleo.

Amesema kwa sasa serikali wanaendelea na tathmini ya kujua nyumba gani imeharibika kabisa na kuona namna ambavyo watawasaidia ili wapate makazi ya kukaaa.

Wakizungumza katika tukio la kupokea msaada huo, baadhi ya waathirika wameishukuru NMB kwa msaada huo na kuwataka wadau wengine kujitokeza ili waweze kuwasaidia mahitaji wakati wanasubiria kupata mwongozo kuhusu makazi yao yaliharibika na maji.

“Tunaishukuru sana NMB kwa kutusaidia huu msaada utatusaidia katika kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama na wanapata chakula maana hapa tuna watoto, waume zetu na wanafunzi hatuna chochote cha kusema tunaweza kutusaidia,” amesema Zuhura Daudi Mhanga wa mafuriko.

Meneja wa Huduma Kwa Wateja  Bank ya  NMB Tawi la Mtwara Fundi Mohammed Fundi akikabidhi sehem ya msaada Kwa waathirika wa mafuriko waliohifadhiwa shule ya Sino Sekondari Mtwara Mikindani





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...