Mchunguzi wa Dawa Katika Maabara ya Microbaolojia wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa  Waridi Shaban akionesha moja sampuli wanayopima kuangalia viwango katika Maabara hiyo wakati waandishi wakiwa katika ziara ya Maabara hiyo.
Mchunguzi wa Dawa wa Maabara ya Microbaolojia wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Waridi Shaban akioneshesha namna uchunguzi uliofanyika na kuonyesha matokeo wakati wa ziara ya waandishi katika Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa Buzuruga mkoani Mwanza.

Baadhi ya dawa za Maji wanazozichuka kwa kununua katika soko na kufanya uchunguzi wa ubora.

 

*Ni pamoja na kutumia maabara ya Macrobaolojia 

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

 MAMLAKA ya ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa imesema kuwa dawa zote zinazotengenezwa ndani na nje za nchi zinazoingia zinachunguzwa ili zisiweze zikaleta madhara kwa wananchi wakati zikiwa katika soko.

Hayo aliyasema Mchunguzi wa Microbaolojia Waridi Shaban wakati wa ziara waandishi kuangalia uwekezaji wa Serikali katika Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa iliyopo Buzuruga mkoani Mwanza.

Shaban amesema dawa kabla haijaingia katika soko wanazipima kuangalia viwango vilivyokuwepo ni vile vinavyoendana na viwango vilivyoidhinishwa kutumika katika dawa.

Amesema kuwa Microbaolojia wanapima hata hali ya mazingira dawa inahifadhiwa kwani bila kufanya hivyo jamii inaweza kupata madhara yanayotokana na ubora wa dawa kutokidhi kutokana na uhifadhi wa dawa usipozingatiwa.

Shaban amesema wakati mwingine dawa zikiwa katika soko Mamlaka inao mfumo wa kuzichukua katika utaratibu wa kununua kama wateja binafsi ambapo wanakuja kuzifanyia uchunguzi.

Hata hivyo amesema maabara ya Microbaolojia ni muhimu katika masuala ya udhibiti wa  dawa, vifaa tiba ma vitendanishi  kwani kuwepo kwake ni suluhisho katika uhakika wa kulinda afya ya jamii.

Shaban amesema kuwa maaba ya  macrobalojia katika uchunguzi huchukua muda mrefu ni kujiridhisha kutokana na sampuli zinazotakiwa kupima kwa kuangalia mambo mbalimbali.

"Tunapima kila kitu kwenye dawa nia ikiwa ni kujiridhisha na tunapobaini dawa hajakidhi viwango haingii katika soko." Amesema Shaban.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...