Na Amir Kilagalila, Njombe

 

WAKATI baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe likikutana na kupitisha makisio na kadirio ya zaidi ya shilingi bilioni 27.7 ya bajeti ya mwaka mpya wa fedha wa 2021/2022, Mkuu wa Wilaya hiyo Lauteri Kanoni ametaka bajeti hiyo ioneshe namna itakavyoshughulikia changamoto za wananchi ikiwemo ukamilishaji wa maboma ya vituo vya kutolea huduma za afya,elimu pamoja na majengo chakavu.

 

Katika kikao maalum cha baraza la madiwani mkuu huyo wa Wilaya amesema ni lazima bajeti hiyo pia iendane na mwelekeo wa ilani ya uchaguzi mkuu na sera mbalimbali huku akitaka ilenge kwenda kushughulikia maboma ya muda mrefu ambayo wananchi wametumia nguvu zao bila mafanikio.

 

“Sera ya nchi kila kijiji kiwe na zahanati,kuna boma lina zaidi ya miaka saba na hakuna kinachoendelea hivyo lazima tuanze ili kukamilisha haya.”Alisema Kanoni

 

Emmanuel Kilundo ni afisa mipango wa halmashauri hiyo,kwa niaba ya mkurugenzi ameweka wazi makisio na makadirio ya bajeti ya shilingi bilioni 27.7 kwa mwaka mpya wa fedha wa 2021/2022 kupitia makusanyo mbalimbali yakiwemo ya mapato ya ndani na fedha toka serikali kuu.

 

“Kuna ujenzi kwa ajili ya nyuma ya mkurugenzi,ujenzi wa hospitali ya wilaya na vifaa tiba,lakini pia kuna fedha kwa ajili ya mfuko wa jamii hivyo kufanya jumla ya mapato tunayoyatarajia kwa mwaka ujao ni shilingi bilioni 27 .7”alisema Kilundo

 

Baadhi ya madiwani akiwemo Annaupendo Gombela,Fredrick Mwalongo na Onesmo Lyandala ambaye ni makamu mwenyekiti wa halamshauri hiyo wanasema jitihada za pamoja zinahitajika ili kufikia malengo ya utekelezaji wa bajeti hiyo.

 

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Agneth Mpangile amesema ni lazima waende kutekeleza bajeti hiyo ili kuongeza mapato ndani ya halmashauri kauli iliyoungwa mkono na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri edesy lukoa.

 

“Tumetoka 1.6 mpaka 2.4 bilinoni katika mapato yetu kwa kweli tunahitaji kujipongeza,kwasababu tumedhamilia maendeleo katika wilaya yetu.” Alisema Agneth Mpangile 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...