LEO January 18, 2021 Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson amefanya ziara katika shule ya Sekondari Iduda iliyopo mkoani Mbeya ambapo amekabidhi jumla ya Shilingi Milioni sitini, laki tano na sabini na nne elfu (60,574,000/-) ambazo ni fedha zote za mfuko wa maendeleo wa jimbo hilo wa mwaka wa fedha 2020-21 ili kusaidia ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika Shule hiyo.

Dr. Tulia amesema,”Kama tunavyofahamu kwamba Wilaya yetu imekuwa na uhaba mkubwa wa shule za Sekondari zenye kidato cha tano na sita na zaidi katika bonde letu la Uyole hakuna hata shule moja hivyo basi leo hii tumekuja hapa baada ya kukubaliana kwamba fedha zote za mfuko wa Jimbo zitaelekezwa hapa Iduda kwa ajili ya ujenzi wa shule.” Amesema.

“Fedha hizo tulizozitoa zinao uwezo wa kujenga madarasa matatu ambayo tutaanza nayo na huo ujenzi utaanza mara moja kwa sababu fedha zipo, Mbeya mjini safari hii tunahitaji maendeleo na hatutarajii kuona mtu wa kutukwamisha. Ndugu zangu niwaombe sana, fedha hizi hazitatosheleza kujenga na kufikia mahitaji yetu yote kwasababu bado tutahitaji pia mabweni hivyo basi tunapaswa kushirikiana kwa umoja wetu kila mmoja anapoweza hata kutoa nguvu kazi ikiwemo kuleta mawe n.k.” Amesema Dr. Tulia.

“Safari hii mtoto aliyeongoza kidato cha nne ametoka hapahapa Mbeya hivyo basi tunataka tuendelee kuweka mazingira mazuri ili kuongeza ushindani mzuri zaidi katika siku za usoni na ikibidi Mbeya tuendelee kuwa vinara wa elimu nchini.” Amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...