Na Woinde Shizza,  Michuzi Tv -ARUSHA

WITO umetolewa kwa  halmashauri hapa nchini pamoja na mamlaka ya mapato (TRA) kufanya kazi usiku na mchana ili kuweza kupunguza wizi wa mapato unaofanywa na baadhi ya watu wasio na nia njema na serikali, pamoja na kuhakikisha wanakomesha ukwepaji wa ulipaji kodi ya mapato.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karatu  John Lusian Mahu wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya baadhi ya wananchi ambao sio waaminifu wanavyoiibia serikali mapato kwa kutorosha vitu usiku.

"Kwa mfano kwenye Wilaya yetu kuna watu wanaenda kuchota mchanga usiku malori kwa malori  wakitegemea saa hizo  hakuna mtu anayewatoza ushuru na kwakweli wanafanikiwa kwa hilo,  vilevile Kuna uvushaji wa samaki kwa sababu sisi tunaziwa linatoa samaki kule Eyasi  wanatoroshea upande wa Singida kwa sababu ya gari kutembea usiku na kufikisha katika masoko na hao ndio wakwepaji wakuu wa ushuru."Aliasema.

Alisema kuwa  wajanja wachache wamekuwa wakitorosha bidhaa ambazo zinapaswa kulipishwa ushuru ambapo wamekuwa wakisafirisha usiku wakitegemea nyakati hizo hakuna  mtu anayeweza kuwakamata na kuwadai ushuru.

Alisema wakwepaji wa ushuru katika halmashauri  ni wengi sana hivyo ni vyema serikali ikaingilia kati na kuwatafutia walinzi wakiwepo mapolisi kwa sababu halmashauri hazina  polisi ambao wafanya kazi ya kukamata wezi hao ambao wanatorosha vitu bila kulipia ushuru.

Aidha aliwataka pia watu wa mamlaka ya mapato Tanzania kuongeza muda wa kufanya kazi na ikiwezekana wafanye kazi usiku na mchana Ili kuweza kuzuia  watu hao wanaolirudisha taifa nyuma kwa  kupoteza mapato  kwa makusudi kabisa.

"Unajua Kama bandarini wameweza kufanya kazi usiku na mchana  yaani masaa 24 kwanini halmashauri zetu zisiweze kufanya kazi usiku na mchana na kuweza kuokoa  fedha hizo    ambazo zinaibiwa  na watu wachache wasio wazalendo kwa nchi yao." Alisema John.

Aliwataka wananchi kuwa waaminifu na kuacha kuiiibia serikali kodi kwani fedha ambazo wanazitoa, zinasaidia kuletea  maendeleo ikiwemo ikiwemo huduma za kijamii  Kama vile  barabara,shule,hospitali, miundombinu ya maji pamoja na mambo mengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...