Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

BODI ya maziwa nchini imekamata tani tatu za maziwa ya unga ya 'Cowbell' yaliyokuwa yanakaribia kuishiwa muda wa matumizi yakiwa yameongezwa muda wa matumizi zaidi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini Noel Byamungu amesema walibaini kitendo hicho katika kiwanda cha Kampuni ya Hawai Limited Kilichopo Keko Chang'ombe wakiwa katika majukumu yao ya ukaguzi na usimamizi wa kuhakikisha wananchi wanapata maziwa bora.

Amesema Maziwa hayo yalitakiwa kumaliza muda wake wa matumizi Mwezi June, Agosti na Oktoba mwaka huu lakini kiwanda hicho kilifanya kitendo cha Kufunga upya maziwa hayo katika vifungashio vipya vinavyoonesha mwisho wa matumizi ya maziwa hayo kuendelea kutumika hadi Mwezi Augusti Mwaka 2022.

Amesema watendaji wamewaachia Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ahemed Suleiman Mohamed pamoja na Meneja uzalishaji Ahmed Amanzi kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kamishina Msaidizi wa Mkoa Kipolisi Temeke Amon Kakwale amesema tayari wanawashikilia watendaji wa Kampuni hiyo.

Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Noel Byamungu akiwa ameshika Kopo la mziwa ya Cowbell wakati walipofanya operesheni na kubaini kuchanganya Maziwa yanayoisha muda na kwenda kupiga alama ya kuongeza muda zaid katika operesheni iliyofanyika jijini Dar es Salaam.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...