Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaj Rajabu Kundya (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021 Mjini Moshi mwishoni mwa wiki huku wageni wengine na wadhamini wakishuhudia.


MSIMU  wa 19 wa mbio  maarufu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021  umezinduliwa Kimkoa Mjini Moshi huku Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Anna Mghwira akiahidi kuendelea kushirikiana na waandaaji na wadhamini wa mbio hizo ili kuzifanya kubwa zaidi na zenye manufaa makubwa kwa mkoa wake na nchi nzima kwa ujumla.

Akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaj Rajabu Kundya katika uzinduzi uliofanyika Kibo Palace Homes, alisema mbio hizo zimesaidia katika kukuza utalii na biashara katika mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania nzima kwa ujumla na yuko tayari kushirikiana na waandaaji kushugulikia changamoto mbalimbali zilizopo ili mbio hizo ziweze kuandikisha idadi kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa  Mghwira mbio hizo zinasajili takriban washiriki 12,000 na waandaaji wanashindwa kuongeza idadi hiyo kutokana na changamoto na barabara kuwa nyembamba.

“Tulishaanza mazungumzo ya namna gani tunaweza kutanua barabara zetu ili mbio hizi ziweze kusajili washiriki wengi zaidi kwani kwa sasa ikifikiwa idadi maalumu waandaaji wanalazimika kufunga usajili ili kuhakikisha wanaendana na matakwa na miongozo ya Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) na pia kijiridhisha kuwa wanaweza kutoa huduma muhimu kama maji, huduma ya kwanza na pia mbio zote zinaanza bila washiriki kusukumana na kukanyagana.'' Amesema.

Pia alitoa pongezi kwa mbio hizo kwa namna zimeendelea kuwaongezea kipato wafanya biashara wa Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla kutokana na biashara kuongezeka wakati wa Kii Marathon ikiwemo suala la utalii wa michezo (sports tourism).Tukio  ambalo huvutia  zaidi  ya wageni  25,000 katika mji wa  Moshi ambao  baadhi  yao  ni  washiriki   na  watazamaji  ambao  pia  hufurahia  vivutio  mbalimbali za  kitalii  na kupromoti shughuli  nyingine  za  kiuchumi  katika  mji  huo.

Kwa  upande  wake  Meneja wa  bia  ya  Kilimanjaro, Irene Mutiganzi  ambaye  pia  ni  meneja  wa  kinywaji  cha  Grand Malt , alisema wanajivunia  kuwa wadhamini wakuu wa  mbio   hizo  kwa  mwaka  wa  19 na kusisitiza kuwa kwao ni jambo la kizalendo  kwani ni shughuli ambayo inautangaza Mkoa wa Kilimanjaro, utalii na kuongeza kipato kwa nchi kwa ujumla.

Aidha  alisema  wamejiandaa  vizuri  kwa  ajili  ya  mbio  za   mwezi ujao  ambapo  wametenga  shilingi  milioni   25  kwa  ajili  ya  zawadi  za  washindi wa  kwanza  kwa  mbio  hizo  kwa  upande  wa wanaume  na  wanawake  ambapo   washindi   watajinyakulia   shs  milioni 4  kila  mmoja   na  watanzania wa kwanza upande wa wanaume na wanawake   watapata   shs  milioni  1.5   kama  motisha  .

Aidha  Irene  pia  amewataka  wale ambao  watapenda  kushiriki kwenye  mbio   za  kilometa  5  nao  wajisajili  mapema   kwani  nafasi  za   ushiriki  zitakuwa  chache   kwa  mara  nyingine  tena.

Naye   Mkurugenzi  wa Tigo Kanda ya Kaskazini  Henry Kinabo, ambaye kampuni yake inadhamini mbio za Km 21 alisema mwaka huu wanatarajia  Tigo Kili Half Marathon  yenye msisimko wa aina yake na burudani . “Usajili kwa njia ya Tigo Pesa umepokewa vizuri  kwani hadi sasa wamejisajii washiriki 3, 917 katika mbio za KM 42, 21 na 5.

Alisema huu ni mwaka wa sita kwao kudhamini Tigo Kili Half Marathon na kama wadhamini wanatoa wito kwa washiriki wendelee kujisajili kwa njia ya Tigo Pesa kwa kuwa ni rahisi na haraka.

Wadhamini wengine ni pamoja na Kilimanjaro Drinking Water, TPC Limited, Unilever Tanzania, Simba Cement, Absa Bank Tanzania  na watoa huduma rasmi Keys Hotel, Garda World Security na CMC Automobiles na bila kuwasahau waandaaji Kilimanjaro Marathon Company na Executive Solutions mbao ni waratibu kitaifa.

Katika  kuongezea  juhudi  za  Serikali za kuzuia Covid 19 kupitia hatua mbalimbali katika maeneo  yote ya  kuingilia  nchini , waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Marathoni watahakikisha  wanafuata miongozo ya serikali.

Hafla ya uzinduzi huo  ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaroaa, Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo, Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA), vilabu mbalimbali, wawakilishi wa wanariadha, wafanyabiashara na vyombo vya habari.

Usajili wa mbio hizo zitakazofanyika Jumapili Februari 28, 2021 katika  Chuo Kikuu cha Ushirika cha Moshi (MoCU), unaendelea kwa njia ya mtandao (www.kilimanjaromarathon.com) na Tigopesa *149*20#


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...