WACHEZAJI  wa Timu ya KMC FC wamerejea kambini tangu wiki iliyopita na leo wataanza mazoezi rasmi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya duru ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajiwa kuendelea Februali 13 mwaka huu.

Aidha katika kipindi hiki ambacho timu zipo mapumzikoni kutokana na michuano ya kombe la CHAN yanayoendelea , kikosi hicho cha wana Kino Boys chini ya kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo kitafanya mazoezi na kucheza mechi nyingi za kirafiki kadiri itakavyoweza ili kuendelea kuwaimarisha zaidi wachezaji.

  Wachezaji ambao tumewaongeza kikosini Charles Ilanfya pamoja na Matheo Anthony wote wapo kambini na watakuwa mazoezini  kujiandaa na duru ya pili ya ligi Kuu soka Tanzania bara katika kuhakikisha kwamba KMC FC inafanya vizuri kwenye michezo yake.

“ Timu ilirejea kambini tangu Januari 18, lakini kutokana na msiba wa kiongozi mwandamizi wa Timu ndugu. Raphael Waryana uliotokea Januari 14 mwaka huu hatukuweza kufanya mazoezi rasmi na kwamba kilichokuwa kinafanyika ni kujiweka sawa, lakini leo tuna anza rasmi mazoezi yetu”.

Itakumbukwa kuwa wachezaji walikuwa mapumzikoni kwa siku 10, na sasa wote wamerejea kambini, isipokuwa wale walioitwa katika Timu ya Taifa ambao ni Juma Kaseja, Israel Patric Mwenda, na wengine ambao hawajarejea ni wale ambao wapo katika Timu ya Taifa ya Vijana U 20, David Brayson, Hassan Kapalata pamoja na Rahim Sheih.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...