Charles James, Michuzi TV

TUMUUNGE Mkono Rais Magufuli! Hii ni kauli iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi alipofika katika Shule ya Msingi Ngai iliyopo Kata ya Mchombe ambapo alijionea uharibifu wa Miundombinu ya shule hiyo na kutoa mchango wake.

Akizungumza na viongozi wa Kata ya Mchombe, Walimu wa Shule ya Msingi Ngai pamoja na wanafunzi, Mbunge Kunambi ametoa kiasi cha Sh Milioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo ambavyo vilititia kutokana na mvua kubwa zilizonyeesha.

Kunambi pia ametoa mchango wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa darasa jipya baadae ya kujionea adha wanayopata wanafunzi wa darasa la sita ambao wanasoma kwenye darasa ambalo upande Mmoja wa ukuta umemeguka.

" Ni lazima kama viongozi wa ngazi ya kata na Jimbo tumsaidie kazi Rais Dk John Magufuli, ninajua changamoto wanazokumban nazo watoto wetu kama tutawaacha waendelee kusoma kwenye mazingira ambayo siyo rafiki, ninatoa kiasi hiki cha fedha ili kiweze kuwezesha ujenzi wa vyoo hivi pamoja na hilo darasa moja ambalo watoto wanasoma licha ya kwamba halina upande mmoja wa ukuta," Amesema Mbunge Kunambi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Aidan Gabriel amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Mbunge Kunambi katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Mlimba huku akimuomba kuendelea kuitupia macho shule hiyo.

" Tunashukuru kwa ujio wa Mbunge wetu, Godwin Kunambi kwa sababu hajaja bure ametuachia mchango wake wa Ujenzi wa vyoo vyetu ambavyo vimetitia, tunampongeza pia kwa moyo wake wa kuchangia ujenzi wa darasa jipya baada ya kuona wadogo zetu wa darasa la sita wakisoma kwenye darasa ambalo liko wazi, sisi tunamuombea kwa Mungu na asichoke kuja kutuona na kutusaidia," Witness Luoga mwanafunzi wa Darasa la Saba.

Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akizungumza baada ya kutembelea Shule ya Msingi Ngai iliyopo Kata ya Mchombe ambapo amechangia Sh Milioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo na mifuko 50 ya saruji ujenzi wa darasa.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi (wa kwanza kushoto) akizungumza na wanafunzi wa darasa la sita ambao ameahidi kuwajengea darasa jipya la kisasa na kwa kuanzia ametoa mifuko 50 ya saruji.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akiwa kazini kusaidiana na mafundi katika ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi Ngai iliyopo kata ya Mchombe.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...