Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

KITUO cha afya MEDWELL kilichopo Halmashauri ya mji Kibaha, mkoani
Pwani kimetoa huduma bure za upasuaji wa mtoto wa jicho kwa zaidi ya
wagonjwa elfu mbili, katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu mwezi
januari 2021.

Pamoja na upasuaji huo  wa mtoto wa Jicho, pia kituo hicho
kimeendesha zoezi maalumu la kutoa matibabu bure  na upimaji wa
magonjwa ya akina mama ikiwa ni  pamoja na upimaji wa saratani ya
mlango wa shingo ya kizazi.

Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Bashiru Khaki,  amesema kambi hiyo ni
ya siku mbili ambapo walilenga kuhudumia wakina mama na jamii.

"Wingi wa wakinamama waliojitokeza kupata vipimo na matibabu baada ya
kutangaziwa kuna huduma hii ya  bila malipo limeonyesha picha kuwa
kuna uhitaji mkubwa wa huduma za afya, hivyo tunajipanga kutoa huduma
hizi mara kwa mara ili wananchi wawe na afya njema na waweze kufanya
kazi na kuinua uchumi wa nchi, alisema.'' Khaki.

Kwa upande wa huduma ya macho pamoja na upasuaji wa mtoto wa Jicho,
mkurugenzi huyo alisema huduma hiyo hutolewa kila siku ya  jumanne na
ijumaa na kuwa  siku zote hutolewa bure.

Amina Ramadhani  Meneja rasilimali watu, anasema zoezi hilo
lilipangwa kufanyika kwa muda wa siku moja lakini kutokana na wingi wa
wagonjwa litafanyika Siku mbili za jumamosi na jumapili.

" Medwel tumejikita zaidi kuhudumia jamii hususani katika suala zima
la afya, hapa tunatoa huduma za vipimo mbalimbali ,xray na ultrasound,
pia upasuaji , huduma za kulaza wagonjwa na nyingine nyingi, pia
tunachimba visima na hata katika suala la elimu pia tunachangia, lengo
ni kuisaidia serikali yetu katika kuimarisha afya ya wananchi wake,"
alisema.'' Amina.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Pwani Dr. Gunini Kamba alipongeza kituo hicho
kwa jinsi kinavyounga mkono juhudi za  serikali katika suala la afya
kwa wananchi wake na kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao pia
akavitaka wadau wengine wa afya wajitokeze kufanya huduma kama hizo.

Mwisho.



NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
Jan 25

KITUO cha afya MEDWELL kilichoko halmashauri ya mji Kibaha ,mkoani
Pwani kimetoa huduma bure za upasuaji wa mtoto wa jicho kwa zaidi ya
wagonjwa elfu mbili ,katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu mwezi
januari 2021.

Pamoja na upasuaji huo  wa mtoto wa JIcho , pia kituo hicho
kimeendesha zoezi maalumu la kutoa matibabu bure  na upimaji wa
magonjwa ya akina mama ikiwa ni  pamoja na upimaji wa saratani ya
mlango wa shingo ya kizazi.

Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Bashiru Khaki,   anasema kambi hiyo ni
ya siku mbili ambapo walilenga kuhudumia wakina mama lakini
walijitokeza ni zaidi ya 400 ambapo hata hivyo wote watapatiwa huduma.

Kwa upande wa huduma ya macho pamoja na upasuaji wa mtoto wa Jicho,
mkurugenzi huyo amesema huduma hiyo hutolewa kila siku ya  jumanne na
ijumaa na kuwa  siku zote hutolewa bure.

Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Dr. Gunini Kamba ,amepongeza kituo hicho
kwa jinsi kinavyounga mkono juhudi za  serikali katika suala la afya
kwa wananchi wake na kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...