Na Mwandishi wetu, Mihambwe

KATIKA kutekeleza kauli mbiu ya Mkuu wa Mkoa Mtwara Mhe. Gelasius
Gasper Byakanwa ya "Ondoa mapori, ongeza uzalishaji" Tarafa ya
Mihambwe imeshiriki mafunzo ya kuondoa mikorosho isiyozaa na namna ya
upandikizaji wa Mikorosho mipya yaliyofanyika leo Ijumaa Januari 22,
2021.

Mafunzo hayo kwa nadharia na vitendo yameongozwa na ofisi ya kilimo
Wilaya kwa uratibu wa ofisi ya Tarafa Mihambwe ambapo Maafisa ugani
pamoja na Wananchi wamefundishwa namna gani ya ukataji miti isiyozaa
na upandikizaji wa miti mipya ya Mikorosho.

Mkulima Mzee Juma Abdallah Chihuka aliishukuru Serikali kuja na
mkakati huu wa kuongeza uzalishaji ambao utakuwa mkombozi wa kiuchumi
kwao.

"Kwa muda mrefu nilikuwa nahitaji elimu hii, naishukuru sana Serikali
ya Rais Magufuli kuingilia kati na sasa tunatarajia uzalishaji
kuongeza kwani Mimi na wenzangu nipo tayari kwa maelekezo na ufanyaji
kazi ilimradi uzalishaji uimarike kama awali." Alisema Mzee Chihuka
akiwa shambani kwake kitongoji cha Shangani kata ya Mihambwe.

Naye Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewasihi Wananchi kote
kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu wa kilimo
ili kuokoa zao la Korosho kwani Serikali ipo pamoja nao kuwapa msaada
wa hali na mali.

"Kwanza niwapongeze ofisi ya kilimo wilaya kwa kuamua kutoka ofisini
na kuja shambani kutoa elimu ya uzalishaji bora wa zao la Korosho.

Pili, kwa  Wananchi waendelee kushikamana na Serikali na kutii
maelekezo ya viongozi wa Serikali na Wataalamu wa kilimo kwani
Serikali ipo kwa ajili yao, jukumu lao kubwa ni kufanya kazi kama
ambavyo tunavyowasisitiza kila siku  na ndani ya muda mfupi wataona
matokeo makubwa ya uzalishaji kuongezeka." Alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo ya mafunzo Gavana Shilatu aliambatana pamoja na timu
ya Wataalamu wa Kilimo toka wilayani, Maafisa ugani wa kata na vijiji,
Watendaji kata na wakataji ambao walishiriki elimu ya nadharia
iliyofanyika ofisi ya Mtendaji kata Mihambwe na baadae elimu ya
vitendo iliyofanyika shambani ikihusisha Wananchi kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...