Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth akisaini mkataba wa kuwa Balozi Jatu Plc (katikati) Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Jatu Plc Mohamed Simbano akimkabidhi tisheti miss Tanzania 2018  kwa ajili kwenda kutoa elimu ya mazungumzo na wanafunzi wa elimu ya juu.

Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth akizungumza kuhusiana na ubalozi wa Jatu Plc, Jijini Dar es Salaam.
Meneja mkuu wa Jatu wa Plc Mohamed simbano akizungumza na waandishi Habari kuhusiana na kutoa ubalozi wa Miss Tanzania 2018  Queen Elizabeth.


*Jatu kutoa elimu ya kunufaisha watanzania 

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

MISS Tanzania 2018  Queen Elizabeth amekula bingo la Balozi wa JATU Plc kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili kuzungumza na vyuo vikuu (Unitalk).

Akizungumza na waandishi Habari wakati wakimtangaza Balozi huyo Meneja Mkuu wa JATU Plc Mohamed Simbano amesema kuwa kuwa na Balozi ni kutaka kuwaunganisha wanafunzi fursa zilizopo JATU kutokana na kuwepo kwa changamoto ya ajira.

Simbano amesema kuwa wanafunzi wanaposoma wakipata elimu wananweza kuwa wakulima au Wakala na kuweza kujiajiri zaidi kuliko kutegemea kuajiriwa.

Simbano amesema JATU wanafunzi wengi wanapokuwa vyuoni hawana elimu kuja kuishi mtaani hivyo wakipata elimu wanavyohitimu wanaweza kujua sehemu ya kuanzia.

Nae Balozi wa JATU Plc Queen Elizabeth amesema wanafunzi wanachangamoto pindi wanapohitimu wanapoingia katika soko la ajira hivyo JATU itafungua fursa.

Amesema JATU kuingia hakuhitaji kuwa na mtaji mkubwa hivyo hata kwa fedha zao wanaweza kuwa sehemu ya Jatu.

Miss Elizabeth amesema wataanza na vyuo 10 wataendelea kutokana na mahitaji yaliyopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...