Jane Edward, Michuzi TV,Arusha

MKUUwa Wilaya ya Arusha Kennan Kihongosi ameishauri Mahakama kutoa elimu  kwa wananchi katika ngazi za chini  ili  kufahamu haki na wajibu wao hasa katika masuala ya kesi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza  katika maadhimisho ya wiki na siku ya sheria nchini yaliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya TBA mkoani Arusha.

Kihongosi aliipongeza mahakama kwa namna ambavyo imeanza kutoa elimu kwa jamii na mashuleni kuhusu haki zao kwani kwa kufanya hivyo kunasaidia Sana kupunguzwa idadi ya mashauri yanayoenda mahakamani kwani migogoro mingi itaishia ngazi za chini.

Kwa upande wake Naibu Msajili mfawidhi wa Mahakama kuu Arusha,Ruth Massam alisema kuwa,katika kuadhimisha wiki hiyo wameanza kutoa elimu katika shule mbalimbali za sekondari na msingi ,katika gereza kuu la Arusha na gereza la watoto ,pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima kwa lengo la kuwapa misaada mbalimbali.

Amesema kuwa,kauli mbiu ya mwaka huu ni "miaka 100 ya mahakama kuu,mchango wa Mahakama katika kujenga nchi inayozingatia Uhuru,haki,udugu amani na ustawi wa wananchi 1921-2021."

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kupata elimu katika viwanja hivyo katika  kuelekea wiki hiyo ambapo watakuwa wakitoa elimu kuhusu sheria za kazi,ardhi,na madalali,elimu kuhusu mirathi,elimu juu ya ndoa na talaka,sheria mbalimbali zinazohusu watoto,sheria za wanyamapori,sheria za uhamiaji ,rushwa na uhujumu uchumi na elimu juu ya mahakama ilivyojikita katika matumizi ya TEHAMA .


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...