MWANASHERIA mkazi wa mkoani Arusha, Isikael Charles ameibuka mshindi wa Jackpot ya kila wiki ya Cheza Pesa inayotoa Milioni 15 kwa washindi.

Isikael miongoni mwa washindi watatu walioingia kwenye fainali ya Jackpot kubwa ameibuka na kitita cha Sh 10 Milioni.

"Sikutarajia kushinda kiasi hiki cha pesa, siamini kilichotokea tena mwanzo huu wa mwaka, pesa hii nitaiweka kwanza benki wakati nikijipanga namna ya kuitumia." alisema Isikael.

Katika droo hiyo, Vicent Jeremiah wa Same alishinda kitita cha Sh 1 milioni na Imani Adamson wa Morogoro aliibuka na kitita cha Sh 3 Milioni.

Kwa nyakati tofauti washindi hao walieleza namna walivyofurahia ushindi huo na kueleza kutumia pesa hizo kuboresha biashara zao.

Cheza Pesa imekuwa ikitoa washindi wa jackport ya kila siku ambao wamekuwa wakijishindia mamilioni kwa kucheza kwa Sh 500 hadi Sh 2000 tu.

"Wote wanaocheza na Cheza Pesa wanaingia kwenye Jackpot kubwa ya kila wiki inayotoa Sh 15 Milioni, ambayo mshindi wa kwanza anaondoka na Sh 10 Milioni, wa pili Milioni 3 na mshindi mwingine Sh 1 milioni," alisema Balozi wa Cheza Pesa, Najma Paul.

Alisema katika Jackpot ya wiki kuna washindi 10 wanaopata bonusi ya Sh 100,000 kila mmoja."Ni rahisi kucheza na kushinda, unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye menyu ya malipo na kwenda kwenye lipa bili kisha weka namba ya kampuni ambayo ni 551551 kisha unaingiza namba zako tano za bahati alafu unaweka kiasi ambacho ni kuanzia Sh 500 hadi 2000 ili kushinda hadi milioni 30,000,000/= kwenye droo ya kila dakika 2."

Alisema washiriki wote katika droo hiyo wanaingia kwenye Jackpot kubwa ya kila Jumapili ambayo inatoa mshindi wa milioni 10, milioni 3, milioni 1 na washindi 10 wa bonusi ya Sh 100,000 kila mmoja. Jackpot hiyo inaruka kupitia ITV na EATV kila jumapili saa tatu na nusu usiku

"Cheza pesa, shinda pesa, hii ndiyo kauli mbiu ya jackport hii, ni rahisi kucheza na kushinda, tukifanya bahati nasibu hii chini ya mwamvuli wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania." alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...