RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeundwa kwa lengo la kuendeleza na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Zanzibar.

Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Amani uliofanyika huko katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mazizini nje kidogo mwa Jiji la Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa  Mkutano huo umefanyika wakati muafaka ambapo nchi imefanikiwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 katika hali ya amani na ulivu mkubwa.

Amesema kwamba suala la kuendeleza na kudumisha amani hapa Zanzibar limepewa kipaumbele katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na mipango ya maendeleo ya Kitaifa.

Rais Dk. Mwinyi aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane itaendelea kufanya kila linalowezekana kwa ajili ya kuendeleza fikra za waasisi wa nchi hii na viongozi waliotangulia katika kudumisha umoja na mshikamano wa wananchi wa Zanzibar.

Aliongeza kuwa ni ukweli usio na shaka kwamba maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi yoyote bila ya kuwepo amani na mshikamano.

Kwa msingi huo, Dk. Mwinyi aliwahimiza viongozi wa vyama na Serikali, viongozi wa dini na madhehebu mbali mbali, vyombo vya habari, wazee na vijana katika jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...