Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

AMEKUWA maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii kupitia jumbe za vichekesho katika lugha ya Kiswahili na Kingereza maarufu kama "Memes", picha yake pekee imekuwa kichekesho katika ukanda wa Afrika.

Nelson Ntombela Raia wa Afrika Kusini, alizaliwa Aprili 6, 1987 huko Kagiso Magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo akiwa mwigizaji na mpenzi wa soka.

Akiwa mtoto wa saba na wa mwisho katika familia yao, wazazi wake walikua na maisha duni na hawakuwa na uwezo wa kumtimizia mahitaji yake hali iliyopelekea Nelson kujiingiza katika magenge ya wahuni na matumizi ya dawa za kulevya hali iliyopelekea kutengwa na baadhi ya watu wake wa karibu.

Akiwa na miaka 16 alikamatwa kwa kuendesha genge la wahuni na kuishia kufungwa katika gereza la Juvenile ambako alikutana na washirika wa magenge ya mtaani na kuchaguliwa kuwa kiongozi wao kabla ya kuachiwa miezi michache badaye.

Hata baada ya kuachiwa Nelson hakuacha maisha ya kuwa na magenge ya kihuni na vibaka, alipofikisha miaka 26 arirudi gerezani kwa makosa ya kuvunja nyumba na kupora.

Akiwa gerezani kwa mara ya pili, Nelson alipata pigo la kuondokewa na Mama yake mzazi jambo lililomfanya abadili mfumo wa maisha baada ya kupoteza nguzo muhimu katika maisha yake, hapo ndipo alipogeukia tabia njema na kuishi maisha huru.

Alipotoka gerezani alipata shavu la kuigiza filamu mbalimbali ikiwemo Rythim City ambayo aliipamba kwa kutumia lugha zinazotumika gerezani pamoja na kutokea katika filamu za Isidingo, Generation, The Legacy na Isithembiso ambapo kupitia filamu alifahamika zaidi kwa jina la Chicken kutokana na tabia yake ya kubeba na kutembea na kuku hai.

Kinachowavutia wengi kuhusu Nelson ni kuendelea kubeba kuku hadi leo pamoja na kuvaa nguo zenye chapa ya mnyama huyo.

Nelson amejaliwa mke na mtoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...