Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MZEE mwenye umri wa miaka 80 aliyefahamika kwa jina la Davis Mabeba amefariki dunia baada ya kwenda nyumba ya kulala wageni katika Hoteli ya Mbezi Garden akiwa na binti mrembo mwenye umri wa miaka 33 aitwaye Neema Kibaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Ramadhan Kingai amewaeleza waandishi wa habari leo Januari 18,2021 kwamba mzee huyo amefariki dunia Januari 16 mwaka huu akiwa kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.

"Januari 16,2021, saa tisa katika Kituo cha Polisi Mabwepande tulipokea taarifa huko Mbezi makonde katika hoteli ya Mbezi Garden kuna mteja amefariki chumbani.Taarifa hizo tulipokea kutoka kwa Meneja wa hoteli hiyo aitwaye Newton Simkonda(44), mkazi wa Ukonga Majohe.

"Aliliambia jeshi la Polisi huko Mbezi Garden hotelini kwake katika Wilaya ya Kipolisi Mabwapande na Mkoa wa kinondoni kuna mteja amefariki dunia chumbani  alipokodi akiwa na mwanamke wake.Baada ya taarifa hiyo kupokelewa Mkuu wa upelelezi Mabwepande  walifika  eneo la tukio na kumkuta mwanamke aitwaye Neema Kibaya(33) mkazi wa Goba Marobo aliyekuwa na marehemu,"amesema Kamanda Kingai.

Ameongeza mwanamke huyo alieleza alifika hotelini hapo Januari 16, saa tisa na  walipokuwa wamekubaliana wakutane na kumkuta marehemu ameshachukua chumba namba 22   akiwa na maji na juice, baada ya kufika aliweza kuagiziwa  chips  na mishikaki  mitatu na mzee huyo.

"Akiwa  anasubiria chips hizo huku wakiwa wanaendelea maandalizi ya tendo la ngono ghafla alimwona marehemu akipumua kwa shida ndipo akatoka kwenda mapokezi kuomba msaada, baada ya taarifa wahudumu waliongozana na   uongozi wa hoteli walifika na kumkuta mzee huyo haongei na hafanyi chochote huku akiwa ametoa macho.

"Ambapo uongozi wa hoteli ulibaini kuwa mteja wao amefariki dunia, ndipo Meneja akachukua jukumu la kutujulisha Polisi na tulipofika eneo la tukio,katika uchunguzi wa awali uliofanyika  mwili wa marehemu haujakutwa na jeraha lolote.Katika  upekuzi marehemu alikutwa na simu aina ya tecno na fedha Sh.37,000,"amesema Kamanda huyo wakati anaelezea kuhusu tukio hilo la kifo.

Amefafanua baada ya polisi kumpekua walimkuta na kitambulisho cha mpiga kura , hivyo kuweza kumtambua marehemu kwa jina la Davis  Makerege Mabeba(80),mkazi wa Goba kwa Ndambi. Mwanamke aliyekuwa na marehemu chumbani   anashikiliwa kituo cha Polisi Goba kwa mahojiano na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...