Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania,  John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini yatakayofanyika Februari Mosi 2021 jijini Dodoma.

Imeelezwa madhimisho hayo yatakayokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 100 ya Mahakama Kuu yatatangulina maonesho ya wiki ya sheri yatakayoanza Januari 23 hadi 29, 2021 kwa maandamano yatakayoongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kutoka Mahakama Kuu Dodoma hadi viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma ameyasema hayo leo Januari 18, 2010 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maadhimisho ya siku ya sheria mwaka huu wa 2021

Aidha Jaji Mkuu amewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kijitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho hayo ili wapate uelewa na msaada wa kisheria.

Pia amewataka wananchi kujenga tabia ya kutafuta taarifa mbalimbali kila inapowezekana badala ya kusubiri taarifa ziwafate walipo.

"Wananchi wasisubiri tu maadhimisho ya wiki ya sheria kupata taarifa mbalimbali za kimahakama, wanaweza kutembelea tovuti ya mahakama na kupata taarifa zote muhimu, watapata taafa za namna ya kufungua mashauri, msaada wa kisheria, elimu ya sheria mbalimbali na maboresho mengine kwa kifupi tu wasisubiri taarifa ziwafate walipo," amesema Jaji Mkuu.

Katika hatua nyingine, Jaji Mkuu amesema, kuanzia Februari mwaka huu mahakama itaanza kutoa  Muhtasari wa hukumu mbalimbali zinazoamuliwa mahakamani kwa lugha ya kiswahili ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuelekea kuendesha shughuli zote za mahakama kwa lugha ya kiswahili.

Amesema, suala la uendeshaji wa shughuli za mahakama kwa lugha ya kiswahili ni suala muhimu lakini linahitaji umakini mkubwa karika kulitekeleza.

"Mwishoni mwa mwaka jana Mheshimiwa Waziri wa sheria alitutembelea, tulizungumza kwa kina kuhusu uendeshwaji wa shughuli zote za mahakana kwa lugha ya kiswahili lakini ni suala linalohitaji umakini mkubwa. Hili suala ni muhimu sana na tayari katika mahakama ya mwanzo shughuli zote zinafanyika katika lugha ya kiswahili," amesema Jaji Mkuu.

Ameongeza, kiswahili kinatumika kwa asilimia 70 katika shughuli za kimahakama kwa sababu mahakama za mwanzo ambazo mashauli yake husikilizwa kiswahili ndizo zinazosikiliza asilimia 70 ya mashauri yote.
 
Amesema katika mahakama nyingine ni kumbukumbu tu za kimahakama ndizo zinaandikwa kiingereza lakini shughuli nyingine zinafanyika kiswahili isipokuwa pale inapolazimu kutumia lugha ya Kiingereza.

Amefafanua kuwa, katika mahakama za Wilaya, Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na Mahakama za Rufani kumbukumbu za mahakama zinaandikwa kwa Kiingereza lakini shughuli za mahakama kama hakuna mawakili zinaendeshwa kwa lugha ya kiswali..,

Ameongeza kuwa walikubaliana na muheshimiwa waziri kwamba suala la kutumika kwa kiswahili mahakamani linahitaji umakini mkubwa kwa sababu wanasheria wamesoma kwa kiingereza na ni Kiingereza cha kitaluma ambacho kinahitaji tafsiri itakayofanya neno likitumika katika hukumu moja ifanane na nyingine kusiwe na tofauti yoyote.

Alisema utekelezaji wa suala hili unatakiwa kuanzia serikalini ambako watatakiwa kubadili sheria kwa kuzitafsiri sheria zote muhimu zinazotumika ili kurahisishia mahakama kuendesha shughuli zake kwa lugha ya kiswahili ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu kwa lugha hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...