Wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wakiwa
Katika kikao Cha RCC hii leo Katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Arusha.

 Na Woinde Shizza ,  Michuzi Tv Arusha

KAMATI ya ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) imepitisha  zaidi ya bilioni
 303 kama mapendekezo ya mpango wa bajeti na makadirio ya mkoa wa
Arusha kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Akisoma mapendekezo ya mpango wa bajeti hiyo katibu tawala wa Mkoa wa
Arusha Richard Kwitega  katika kikao cha kamati hiyo alisema kuwa
sekretariet ya mkoa imeanza rasmi mandalizi ya mpango wa bajeti ambao
unahusisha hatua muhimu ambazo ni kubainisha vipaumbele vya
mpango,bajeti na mikakati yake pamoja na kuandaa bajeti ya taasisi kwa
kuzingatia ukomo wa bajeti ya serikali.

Alieleza kuwa utekelezaji wa bajeti ya mkoa 2021/2022 utazingatia
vipaumbele vya mkoa ambavyo ni kuendelea na uimarishaji wa elimu ya
msingi na sekondari katika ngazi zote kwa kuimarisha mazingira ya
kujifunzia na kufundishia, kuboresha huduma za afya ya kinga na tiba
katika ngazi zote kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya afya,
kuimarisha upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba ikiwa ni pamoja na
kuwajengea uwezo watumishi wa afya.

Alieleza kuwa vipaumbele vingine ni kuimarisha upatikanaji wa huduma
ya maji safi na maji taka kwa kujenga miundombinu mipya na kufanya
ukarabati wa miundombinu iliyopo, kuimarisha pato la mkulima kwa
kuongeza tija katika umaoishaji wa mazao, kuongeza thamani ya mazao na
kuimarisha mfumo wa huduma za ugani.

Alisema katika kuimarisha pato la mkulima pia wataendeleza kilimo cha
umwagiliaji kwa kujenga na kukarabati mifumo ya umwagiliaji husanI
katika Bonde la Eyasi,kuimarisha miundombinu na utafutaji wa masoko
pamoja na kuongeza matumizi ya pembejeo na zana bora za kilimo.

Kwa upande wa mifugo Kwitega alisema kuwa wataporesha afya za mifugo
kwa njia ya chanjo dhidi ya magonjwa, kuimarisha miundombinu ya
ufugaji, kuimarisha mazao ya mifugo na uvuvi pamoja na kutenga maeneo
mahususi ya malisho kwaajili ya wafugaji.

Alibainisha vipaumbele vingine kuwa  ni kuimarisha sekta ya viwanda
kwa kutenga maeneo ya uanzishwaji wa viwanda na kuboresha mazingira ya
uwekezaji na biashara, kuimarisha miundombinu ya utalii kwa
kuhamasisha utalii wa ndani ukiwemo utalii wa mambo ya kale, kuweka
vivutio kwa watalii ili kuongeza siku za kufanya utalii mkoani Arusha
paoja na kuipatia ufumbuzi migogoro yote inayojitokeza kati ya
wananchi na wanaoishi maeneo ya jirani na hifadhi na mamlaka husika.

kuimarisha ukusanyaji wa kodi na  mapato ya serikali kwa kubuni vyanzo
vipya na endelevu vya mapato, kuendeleza utoaji wa elimu kwa walipa
kodi na ushuru pamoja na kuongeza usimamizi wa ukusanyaji wa mapato
kutoka kutoka vyanzo vilivyopo, nyingine ni kuimarisha wa sera ya
uwekezaji wa wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa vikundi vya
wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Katika utoaji wa mikopo kwa vikundi pia wataimarisha ufuatiliaji wa
mikopo na kutoa elimu juu ya uanzishaji na uendelezaji wa biashara na
ushauri kuhusu matumizi endelevu ya mkopo, nyingine ikiwa ni kuongeza
tija na ufanisi wa kazi kwa watumishi kwa kufanya ajira mpya,
upandishaji wa vyeo na madaraja  ulipaji wa madeni ya watumishi pamoja
na stahili za kisheria na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.

Aidha alisema kuwa katika kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele hivyo
mkoa unatarajia kutumia jumla ya shilingi bilioni 303,172,660,428 kwa
matumizi ya kawaida na maendeleo ambapo mishara ya wstumishi ni
178,059,162,00 miradi ya maendeleo 71,041,303,428, matumizi mengineyo
11,480,490,000 pamoja na mapato ya ndani ya halmashauri
42,591,705,000.

Sambamba na hayo pia alieleza mchanganuo wa makadirio ya ukusanyaji wa
mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo halmashauri ya
Arusha jiji inataraiwa kukusanya 22,099,965,000, Arusha DC
4,219,640,000, Karatu 4, 501,993,000, Longido DC 2,208,158,000, Meru
DC 4, 049,395,000, Monduli 2,677,908,000 pamoja na Ngorongoro
2,834,646,000 jumla ikiwa ni Bilioni 42, 591,705,000 ambapo  mchango
wa halmashauri kwenye miradi ya maendeo ni billioni 3,239,601,827.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...