Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imetoa Sh Milioni 998 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa  mradi maji  utakaowezesha kumaliza tatizo la maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha zaidi ya Lita za Maji Milioni 2.5 na kufanya mji wa Chamwino kuondokana na adha ya kukosa maji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kutembelea mradi huo Waziri wa Maji Juma Aweso amesema lengo la kuongeza uchimbaji wa visima ni kupunguza tatizo la maji ambalo kwasasa inalikabili Jiji la Dodoma.

“Nimeona nitembelee mradi huu wa maji kujionea hatua iliyofikiwa na mkandarasi, tunataka mradi huu ukamilike kwa wakati ili wananchi wasiwe wanapata tabu kama wanayoipata sasa," Amesema Waziri Aweso.

Ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA) kuhakikisha kipindi hiki cha vikao vya Bunge huduma ya maji inaboreshwa na kugawiwa kwa usawa.

Amesema Maji yaliyopo sasa yagawiwe kwa wananchi kwa usawa pasipo upendeleo wowote.

“Maji yanayopatikana sasa yagawiwe kwa usawa pasipo upendeleo sio mtaa mmoja wanapata maji kila siku sehemu nyingine hakuna maji inakuwa sio sahihi, kila mwananchi anataka maji na maji hayana mbadala hivyo DUWASA  mhakikishe kipindi hiki cha bunge maji yanatolewa kwa haki na usawa," Amesema Aweso.

Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo Mhandisi Hashimu Mayunga amesema mradi huo unatekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na unatarajia kukamilika februari 28 mwaka huu.

Amesema maji yatakayopatikana yatahudumia wananchi wa chamwino.

“Tunatarajia kukamilisha mradi huu ndani ya muda tuliopangiwa huvyo imetulazimu kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha inapofika muda huo tayari kazi iwe imemalizika” Amesema.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma,Dk Bilinith Mahenge amesema ni vyema kuibua vyanzo vipya vya maji ilikumaliza changamoto ya maji ambayo hivi sasa inakabili mkoa wa Dodoma.

Amesema Dodoma sasa ni makao makuu ya Nchi hivyo idadi ya watu inaongezeka siku hadi siku  na matumizi ya maji yanaongezeka hivyo DUWASA wanatakiwa kubuni miradi mipya ambayo itazalisha maji.

“Dodoma ni makao makuu ya nchi na serikali na huduma ya maji ni sekta muhimu sana kwani haina mbadala naomba mamlaka inayohusika kuangalia namna ya kuzalisha vyanzo vipya vya maji vitakavyosaidia kumaliza tatizo la maji”Amesema Dk Mahenge.

Wazi wa Maji, Juma Aweso akikagua mradi wa maji unaojengwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Mkandarasi wa Mradi wa Maji unaojengwa Wilayani Chamwino, Mhandisi Hashimu Mayunga akimpa maelezo ya mradi huo Waziri wa Maji, Juma Aweso alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo.
 
Waziri wa Maji, Juma Aweso akizungumza na wandishi wa habari baada ya kukagua miradi ya maji wilayani Chamwino mkoani Dodoma Leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...