Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile, akiwasilisha taarifa ya Wizara yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) Bungeni, Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso na wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso akizungumza baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) kuwasilisha taarifa ya Wizara yake kwa wajumbe wa Kamati hiyo, Bungeni, Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akifafanua huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Ritta Kabati (aliyesimama katikati) kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma baada ya kikao cha Wizara hiyo na wajumbe wa Kamati hiyo. Kushoto ni Meneja wa T-PESA, Lulu Mkude

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne Kilango Malecela (wa kwanza kushoto) na wajumbe wa Kamati hiyo wakifurahia jambo wakati Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) akifafanua jambo kwa Kamati hiyo alipowasilisha taarifa ya majukumu ya Wizara yake Bungeni, Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso (wa tatu kushoto aliyeketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia), Naibu Waziri, Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia) na Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula (wa pili kushoto) na wajumbe wa Kamati hiyo waliosimama mbele ya banda la TTCL baada ya kikao chao Bungeni, Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso (wa tatu kushoto aliyeketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) na wakuu wa taasisi za Wizara hiyo waliosimama mbele ya banda la TTCL baada ya kikao chao Bungeni, Dodoma. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Mhandisi Kundo Mathew na wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Zainab Chaula.

*************************************************

  • Miamala Milioni 300 Inafanyika Kwa Mwezi Mtandaoni
  • Serikali Yapata Bilioni 80 kwa Mwezi Ya Tozo na Kodi kutoka Kwenye Mitandao
  • Serikali Kuandaa Ramani ya Njia ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano

Na Prisca Ulomi, WMTH

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameiarifu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa kiasi cha shilingi trilioni 18 zinapita kwenye mitandao kwa mwezi wakati wa kikao chake na kamati hiyo kilichohudhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na wakuu wa taasisi zake ikiwemo Shirika la Posta Tanzania (TPC), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA -CCC) na Tume ya TEHAMA (ICTC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma

Dkt. Ndugulile amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa kiasi cha miamala milioni 300 inafanyika kwa mwezi mtandaoni na Serikali inapata shilingi bilioni 80 kwa mwezi za tozo kutokana na fedha zinazopita mtandaoni na mzunguko huo wa fedha mtandaoni kwa mwezi, miamala inayofanyika na tozo ambazo Serikali inapata ni kutokana na kuwepo kwa matumizi ya TEHAMA

Amefafanua kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni njia kuu ya uchumi na inawezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano yenye kasi, kufanikisha utendaji kazi wa mifumo ya TEHAMA na huduma za fedha mtandaoni ambapo Wizara imejipanga kuandaa ramani ya njia ya  miundombinu huo ili kufanikisha mwingiliano wa ujenzi na upanuzi wake pale inapokutana na njia za miundombinu mingine kama vile ya barabara, maji, umeme na reli

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuongeza udhibiti na usimamizi wa huduma za mawasiliano kwenye suala la fedha mtandao ili kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuweza kuongeza mchango wa tozo Serikalini zaidi ya shilingi bilioni 80 kwa mwezi kwa kuwa miamala mingi ya fedha inafanyika na fedha nyingi zinapita kwenye mtandao ili TEHAMA iongeze mchango wake kwenye ukuaji wa uchumi na kuchangia zaidi pato la taifa

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa Wizara itaipa ushirikiano wa kutosha Kamati hiyo ili kwa pamoja Serikali kupitia Wizara hii na Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wote kwa pamoja wanamhudumia mwananchi

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Wizara itaendelea kusimamia na kuendesha vema Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za mawasiliano na TEHAMA inatumika kurahisisha maisha yao ya kila siku katika nyanja ya kiuchumi na kijamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...