Punde chumba chetu cha habari kimezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Ilunga Khalifa almaarufu 'C Pwaa' ambaye amefariki alfajiri ya kuamkia leo akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taarifa rasmi kutoka kwa ndugu wa karibu wa C Pwaa zinathibitisha CP kuugua ugonjwa wa Nimonia na alifikishwa hospitalini hapo kwa matibabu, hali yake haikuwa njema hadi umauti unamkuta alfajiri ya leo.

Aidha taarifa kutoka kwa mtu wake wa karibu zinaeleza kuwa msiba upo Magomeni Mikumi na kwamba maziko yake yatafanyika saa kumi.

Uongozi wa MICHUZI MEDIA unaungana na Ndugu,jamaa na marafiki na Watanzania wote kwa ujumla  kuomboleza kifo cha 'Lijendari' huyu katika anga ya muziki wa Kizazi kipya.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...