Mbio maarufu za Tigo Kilimanjaro Half Marathon 2021 zimezinduliwa rasmi kimkoa katika viwanja vya Kibo Palace Homes, Mjini Moshi kwa kushirikisha viongozi mbalimbali, wadhamini, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA), waandaaji wa mbio hizo na wadau mbalimbali.
Akizindua mbio hizo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Alhajj Rajab Kundya aliwapongeza wadhamnini na waandaaji wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager 42km, Tigo-21km Grand Malt 5km na wadhamini wengine wa meza za maji kwa kazi nzuri na kusema wamezifanya mbio hizi ziwe maarufu zaidi na pia wameendelea kuutagaza Mkoa wake wa Kilimanjaro. 

Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa aliipongeza kampuni ya Tigo kwa kutoa hamasa kwa watanzania .

“Hii iwe changamoto kuwafanya watanzania wakimbie kwakasi zaidi ili washinde hata zawadi nyingine kubwa zinazotolewa na waandaaji.

Alitoa wito kwa wafanya biashara kutumia fursa hii vizuri kwani wakati huu wa Kilimanjaro Marathon ndio muda wa kufanya biashara tofauti tofauti. “Wenye mahoteli anzeni kufikiria kutoa ofa mbalimbali ili washiriki watenge muda zaidi wa kukimbia lakini pia kufanya utalii na wenye mabaa na makampuni mbalimbali mnaweza kuandaa promosheni ya wiki nzima kutangaza biashara zenu 

Alipongeza wadhamini wengine wakiwemo KK Security, Keys Hotel, Kilimanjaro Water, TPC Sugar, Simba Cement, AAR, Kibo Palace, Barclays Bank na Precision Air na waandaaji Wild Frontiers, Deep Blue Media na Executive Solutions ambao ni waratibu wa kitaifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja Chapa wa TBL, Irene Mutiganzi alisema Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kudhamini mbio hizo kwa miaka 19 sasa kutokana na weledi na uzoefu mkubwa wa waandaaji ambao wamefanya mbio hizo ziwe maarufu sana na moja ya matokeo makubwa nchini huku mwaka huu kauli mbiu ikiwa ‘Twenzetu Kili.’

Alisema kwa mwaka huu, Kilimanjaro Premium Lager imejiandaa vizuri kwani itatoa zawadi zenye thamani ya Tsh milioni 20 ambapo mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 42 kwa upande wa mshiriki mwanaume na mwanamke watapata tsh milioni 4 kila mmoja lakini pia imetoa ofa ya milioni tano kwa watanzania watakaomaliza wa kwanza na wa pili ambapo mwanaume wa kwanza na mwanamke watapata sh milioni 1.5 kila mmoja na wa pili watapata Sh milioni 1 kila mmoja.

Alisema mbio maarufu zakilometa 5 maarufu kama Fun Run, zinazodhaminiwa na Grand Malt pia zitafanyika ambapo watu wa rika zote wanaruhusiwa kushiriki. “Hizi ni mbio za kujifurahisha kwa hivyo watu wa rika zote wanakaribishwa kushiriki ili pia iwe kama sehemmu ya mazoezi huku wakipata kinywaji chao cha Grand malt chenye afya tele,” alisema na kuongeza kwa mbio hizo zimeendelea kuwa maarufu. 


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema: “Tigo tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio maarufu za Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa sita mfululizo. Tukiongoza sokoni kwenye mageuzi ya maisha ya kidijiti yakiwamo masuala ya fedha, tunafurahi kwa mara nyingine tena kuwezesha usajili na malipo kwa washiriki kwenye mashindano hayo yajayo kupitia kwa huduma zetu kamilifu za fedha - Tigo Pesa. 

Alisema kwamba kwa miaka kadhaa sasa, Tigo Pesa imethibitishwa kuwa bora zaidi na mfumo wa kuaminika wa malipo kwa wanariadha wote wenye nia kutoka sehemu yoyote nchini. “Zaidi ya hapo, tunakaribisha kila mmoja kwa ajili ya kupata kumbukumbu za mashindano hayo na kutumia wengine kupitia mtandao wenye kasi zaidi Tanzania wa 4G+,” akasema.

Kinabo pia aliendelea kusema, kwamba hadi kufikia leo tarehe 22 Januari 2021, waliokwisha kujisajili ni wakimbiaji 4039, katika full marathon(45km) ni 310, Tigo Kili Half marathon ni 3,469 na Fun Run(5km)-260. Usajili bado unaendelea 

Tumeandaa 12.5 tshs million kwaajili ya washindi 10 wa kwanza upande wa wanaume na wanawake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...