Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Sebastian Kitiku (Mwenye miwani) akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa vituo vya kijamii vya malezi, makuzi na amendeleo ya awali ya mtoto Walayani Chamwino.

 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Sebastian Kitiku (mwenye miwani) akikagua ujenzi wa Kituo cha kijamii cha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kilichopo katika Shule ya Msingi Chamwino mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Sebastian Kitiku (mwenye miwani) akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa vituo vya kijamii vya malezi, makuzi na amendeleo ya awali ya mtoto Walayani humo.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Sebastian Kitiku (mwenye miwani) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha kijamii cha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kilichopo katika Shule ya Msingi KIbaigwa mkoani Dodoma.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

……………………………………………………………………………

 Na Mwandishi  wetu, Dodoma

Vituo vya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika jamii Inaelezwa kuwa vinaweza kuwa suluhisho la changamoto zinazojitokeza katika jamii mbalimbali Nchini ikiwemo mmomonyoko wa maadili kwa watoto.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Sebastian Kitiku wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Vituo hivyo katika Halmashauri za Wilaya nne zilizopo Mkoani Dodoma.

Kitiku amesema Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamaii iliona umuhiu wa wa vituo vya malezi, makuzi na amendeleo ya awali ya mtoto kwa ngazi za kijamii ili kusaidia wazazi na walezi katika maeneo  husika kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi huku wakiwa na uhakika wa malezi ya Watoto wao.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa vituo hivyo vitamilikiwa na kusimamiwa jamii na husika ambayo pia itakuwa na jukumu la kuanzisha vikundi vya malezi kwa lengo la kuiwezesha jamii kuwa na malezi Chanya kwa watoto.

“Hivi Vituo vitatusaidia katika kutoa elimu ya Malezi kwa wazazi na Watoto pia kwani vikundi vya Malezi vya wazazi vitaanzishwa ili kuendana na uendeshaji wa Vituo hivi” alisema

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kogwa Dkt. Omary Nkulo amesema vituo hivyo vya malezi , Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ni muhimu sana katika jamii na vitasaidia jamii kuwa na mahali salama kwa malezi ya watoto.

Amesema hatua hii ikiungwa mkono na jamii, itasaidia kuunga Mkono Juhudi jitihada za Serikali kuchochea uchumi wa viwanda ulioiwezesha kufikia Uchumi wa kati.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Chamwino Peter Simba amesema kituo cha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto kijijini hapo ni neema ya pekee kwao kama kijiji na hivyo watahakikisha wanashirikiana na wadau kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ili kitoe huduma inayokusudiwa.

Kwa Upande wake Afisa Mradi kutoka Shirika la Brac, Pius Ulaya amesema Shirika Llinaunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi wake kupitia ujenzi wa Vituo hivyo katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam ili kusaidia jamii kuondokana na changamoto ya watoto kukosa sehemu sahihi za kujifunza na kupata malezi pale wazazi wanapokuwa katika shughuli za Maendeleo.

Serikali kupitia Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo imebaini changamoto za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto na kuanzisha Mradi wa ujenzi wa Vituo hivyo unaochangiwa na wananchi wa maeneo husika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...