Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, George Lugata (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu mpya za kisasa aina ya Tecno RC6 (Tecno Babkubwa) inayokuja na ofa maalum ya GB 60 bure kwa mwaka mzima, na Itel AC13 (Itel Kitonga) yenye ofa ya GB 48 kwa mwaka mzima, ambazo zitapatikana kwenye maduka yote ya Vodacom nchini. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Itel, Fernando Wolle.

======  =======  ========

 Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania PLC inaendelea kuongoza matarajio yake ya kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali kwa kutoa GB za bure kwa mtu yeyote ambaye atanunua mojawapo kati ya simujanja  mbili mpya zilizozinduliwa leo sokoni, kwa lengo la kuongeza idadi ya vifaa bora vinavyowezesha upatikanaji wa huduma za kidijitali.

Simu hizo mbili, ambazo ni Tecno RC6 (Tecno Babkubwa) zinakuja na ofa maalum ya GB 60 bure kwa miezi 12, wakati ofa kwa Itel AC13 (Itel Kitonga) ni GB 48 bure kwa miezi 12, zote kutoka Vodacom Tanzania PLC.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom, George Lugata, alisema ili kufanikisha maono ya Vodacom ya kuiweka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, "ni lazima tuhakikishe kuwa wateja wetu wanapata huduma za Mtandao na mawasiliano kwa bei nafuu na ubora bila kizuizi chochote," alisema.

“Umuhimu wa mtandao wenye kasi kwa kila mtumiaji wa simu janja unajulikana, mikutano ya skype, kupakua maudhui ya elimu, manunuzi kupitia simu za mkononi na mikutano ya biashara, nikitaja kwa uchache. Na ili watanzania wasiwe nyuma katika ukuaji wa teknolojia, tunahitaji huduma za mtandao wenye kasi na uhakika kila siku na kwa kila simu bora tunayozindua, kwa sababu hiyo tuliamua kutoa GB za bure kwa wale wote watakaonunua simujanja hizi,” alifafanua Lugata.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Tecno Eric Mkomoya, alisema kuwa simu aina ya Tecno RC6 (Tecno Babkubwa) inakuja na kioo chenye ukubwa wa inchi 5, mfumo wa uendeshaji wa Android 10.0, 2000 mAh Li-Ion, betri inayowezesha matumizi ya muda mrefu na imewezeshwa kutumia mfumo wa mtandao wa 4G. Vipengele vya ziada ni pamoja na usalama wa kufungua simu kwa kutumia sura ya mteja na inauzwa kwa shilingi 95,000.

"Na simu yetu ya Itel AC13 (Itel Kitonga) inakuja na sura  ya ukubwa wa inchi 4, 10.0 mfumo wa uendeshaji wa Android, betri ya Li-Ion ya 1500mAh pamoja na mfumo wa mtandao wa 3G, ambapo bei yake itakuwa ni shilingi 75,000," alisema Meneja Uhusiano wa Itel Fernando Wolle.

Lugata alibainisha kuwa uzinduzi wa kampeni ya 'Huku Slopu Tu' inakusudia kuhakikisha kuwa wateja wa Vodacom wanaendelea kuwasiliana, kufanya malipo na kushiriki katika  huduma za kidijitali kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Vodacom Tanzania Plc, Itel na Tecno wamekuwa washirika kwa muda mrefu tangu kuzinduliwa rasmi kwa vifaa vya simu janja nchini. Kampuni hizi zimekuwa zikifanya kazi pamoja ili kuleta mapinduzi katika tasnia ya mawasiliano nchini.

Simujanja za Tecno BabKubwa na Itel Kitonga zinapatikana katika maduka yote ya Vodacom yaliyopo katika maeneo yote nchini. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...