Na Woinde Shizza , Michuzi Tv


KESI inayowakabili askari watatu na raia watano akiwemo Mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite Jijini Arusha Lucas Mdeme(46)leo imechukua sura mpya baada ya askari wa Magereza Kuzuia waandishi kufanya kazi zao ikiwemo kupiga picha wakati taratibu zote za kupiga picha zikifuatwa.

Askari hao na raia hao ambao  wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwemo uhujumu uchumi ,utakatishaji fedha haramu na kupanga njama za kujipatia fedha ya awali Sh.milioni 10 kati ya Sh.milioni 30 walizohitaji kutoka kwa mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite, Sammy Mollel.

Ambapo kesi hiyo ilitajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Wilaya ya Arusha na kuhairishwa hadi Februali 10 mwaka huu kwa madai ya upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.  

Waendesha mashtaka wa Serikali Adelaide Kassalay na Agnes Hyera walimweleza Hakimu Ngoka kuwa wanaomba tarahe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo kwani upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na ndipo Hakimu alipoihairisha hadi tarehe hiyo na watuhumiwa kuendelea kukaa rumande gerezani kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana na mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Kabla ya kupandishwa kizimbani utaratibu mahakamani hapo ulibadilika na raia wote wenye kesi na wasiokuwa na kesi waliamuriwa na askari magereza kukaa nje ya geti la Mahakama na waandishi kuzuiwa kupiga picha na kuzuiwa kuingia ndani ya geti hilo.

Kasheshe hiyo ilimkumba mwandishi wa kike wa gazeti la Mwananchi Husna Issa kwani alipopiga picha alikamatwa na askari magereza wa kiume na kufuta picha zote walizopigwa watuhumiwa hao na kukalishwa chini ya ulinzi na baadae  kutolewa nje ya geti na kukutwa akipata kibano kutoka kwa ndugu wa watuhumiwa hao na kuambiwa kuwa asirudie tena kwani wenyewe wameshaweka mazingira ya ndugu zao kutopigwa picha tena.

" Mmezidi kiherehere mnapiga picha tu waume zetu umeona  Cha Moto sasa!! Angalia watu wameshaweka mambo yao sawa nyie mnataka kuharibu haya sasa " alisikika ndugu akitamba mahakamani hapo

 Akizungumza kuhusu tukio hilo kwa njia ya simu ya mkononi, Mkuu huyo wa Magereza Mkoa wa Arusha Widson Mwanangwa amesema hana taarifa zozote ila atafuatilia kujua ukweli ili hatua zingine zichukuliwe kwani kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa.

Hata hivyo kabla ya kupandishwa kizimbani askari watatu walishtakiwa kijeshi na walibainika na tuhuma na fukuzwa kazi kwa rushwa na waliopandishwa kizimbani ni pamoja na pamoja na  Askari mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi  aliyekuwa Askari kitengo cha Intelijensia Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam,H.125 PC Gasper Paul kitengo Cha Intelijensia Makao Makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa Askari wa kawaida Mkoani Dodoma.

Raia wengine walioshtakiwa  mahakamani mbali ya Mdeme kuwa ni pamoja na Joseph Chacha(43)maarufu kwa jina la ‘’baba Ngodo’’ mkazi wa Ilboru,Leonila Joseph)46) mkazi wa Ilboru,Mfanyabishara maarufu Jijini Arusha ,Nelson Lyimo(58) mkazi wa Kijenge Juu na Omary Alphonce(43)maarufu kwa jina la Matelephone mkazi wa Olasiva Jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...