Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na watendaji
wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya siku moja
katika mkoa huo tarehe 25 Januari 2021. Wa pili kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga na kulia ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi
mkoa wa Simiyu Essau Mawakatumbula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula akikabidhi Hati ya Ardhi kwa Wenza Ramadhani na Martha
Zongo wakazi wa Bariadi mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya siku moja
katika mkoa huo tarehe 25 Januari 2021. kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Bariadi Festo Kiswaga.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na
wananchi wa Bariadi mkoa wa Simiyu aliowakabidhi Hati za Ardhi wakati
wa ziara yake ya siku moja katika mkoa huo tarehe 25 Januari 2021. Wa
pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga na wa pili
kulia ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Simiyu Essau Mwakatumbula.

Meneja Uhusiano na Huduma za Jamii wa Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) Muungano Saguya akifafanua jambo katika Ofisi ya mkuu wa
mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kukagua utendaji kazi wa sekta
ya ardhi katika mkoa huo tarehe 25 Januari 2021.
 


Na Munir Shemweta, WANMM SIMIYU

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula amewaagiza Maafisa Ardhi katika halmashauri nchini kuanza
kufatilia umiliki wa ardhi na wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango wa ardhi
kwa mujibu wa sheria.

Mmiliki yeyote wa ardhi anapaswa kulipa kodi ya pango la ardhi ikiwa
ni sehemu ya utekelezaji wa masharti ya umiliki kwa mujibu wa kifungu
33 (1) cha sheria ya ardhi Na 4 ya mwaka 1999.

Aidha, kifungu cha 48(1) (g) kinaelekeza kuwa kodi ya ardhi isipolipwa
kwa kipindi cha miezi sita mara baada ya mmiliki kutumiwa ilani ya
madai mmiliki huyo anaweza kufutiwa milki yake.

Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika Mkoa wa Simiyu tarehe 25
Januari 2021 kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi
ya pango la ardhi na kuzungunza na watendaji wa sekta ya ardhi, Naibu
Waziri wa Ardhi aliwaelekeza wataalamu wa sekta ya ardhi kuhakikisha
wanatekeleza matakwa hayo ya kisheria Na 4 ya mwaka 1999 kwa
kuisimamia vyema.

"Nawaagiza Maafisa Ardhi katika halmashauri zote kuhakikisha sheria
inachukua mkondo wake na msiendelee kuwalea wadaiwa sugu wa kodi ya
ardhi na mzingatie sheria Na 4 ya ardhi wakati mnatekeleza majukumu
yenu ikiwemo kufuta umiliki baada ya miezi sita kwa wadaiwa." alisema
Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula aliwataka Wakurugenzi katika halmashauri za mkoa wa Simiyu
kuzitumia vyema idara za ardhi katika masuala yote yanayohusu ardhi
ikiwemo upangaji wa miji kwa kuwa mamlaka za upangaji ziko chini ya
halmashauri hizo na kusisitiza kuwa wakurugenzi hao wasipozitumia
vyema idara za ardhi kuna hatari ya kuendelea kwa ujenzi holela.

Aidha, Dkt Mabula ameonesha kutoridhishwa na kasi ndogo ya ukusanyaji
kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Simiyu ambapo hadi sasa mkoa huo
umekusanya shilingi 87,654,120 sawa na asilimia 24 huku mkoa ukidai
zaidi ya Bilioni 5.5 kutoka kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi katika mkoa wa Simiyu Essau
Mwakatumbula alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula kuwa ofisi
yake itahakikisha inaongeza kasi ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya
ardhi ili iweze  kukusanya madeni na kufikia malengo ya makusanyo ya
kodi ya ardhi iliyojiwekea.

Hata hivyo, alisema pamoja na jitihada za mkoa katika kuhakikisha
wadaiwa wote wa kodi ya ardhi wanalipa kuna changamoto kwa baadhi ya
taasisi kutoonesha jitihada zozote za kulipa na kutolea mfano wa VETA,
SIDO na SHIRECU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...