Jane Edward, Michuzi TV- Arusha 

WADAU mbalimbali wa michezo barani Afrika wametakiwa kujitokeza katika tamasha la Sanaa  lijulikanalo kama KAN Festival, lenye lengo la kukutanisha waafrika na kujadili masuala  mbalimbali ikiwemo Sanaa na  maendeleo .

Akizungumza na waandishi wa Habari mratibu wa tamasha  hilo Khalila Mbowe amesema tamasha hilo  litawaleta Pamoja maelfu ya washiriki kutoka katika mitandao, huku akitaja kuwa riadha ni moja kati ya mchezo unayaotarajiwa kuwa kivutio kikubwa.

Alisema kuwa, Tamasha hilo limelenga kuleta mabadiliko makubwa kwa wananchi wa Arusha hususani vijana ambao wataweza kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo kujifunza kupitia bunifu mbalimbali zitakazoonyeshwa kwenye tamasha hilo.

Kaimu Mkurugenzi wa taasisi  ya maendeleo ya MS_TCDC  ambao ndio waandaji wa  tamasha hilo Sara Ezra alisema kupitia tamasha hilo Tanzania itapata uzoefu kutoka nchi nyingine katika maendeleo ya  masuala ya Sanaa na michezo.

Sara alisema kuwa, Tamasha hilo ni mara ya tatu kufanyiwa katika chuo hicho ambapo limeleta manufaa makubwa Sana kwa kutoa elimu kwa vijana na kujifunza kupitia bunifu mbalimbali.

Amewataka wananchi mbalimbali wa jiji la Arusha kuhudhuria kwa wingi katika tamasha hilo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wasanii  mbalimbali kwenye tamasha hilo.

Mmoja wa wasanii Editha Gyindo alisema kuwa tamasha hilo limeweza kuwaleta pamoja wasanii mbalimbali ikiwemo, kundi la Weusi,wasanii wauchoraji, pamoja na wadau ambapo wataweza kujifunza maswala mbalimbali.

        

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...