Mkurugenzi wa shule za St. Mary's nchini Dkt. Rose Rwakatare akizungumza mara baada ya kumalizika kwa misa ya shukrani iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto na  kuhudhuriwa na wanafunzi wa shule hizo waliofika kushukuru kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani yao, Dkt. Rose amewashukuru walimu wa shule hizo na kusema kuwa daima wapo tayari kuwahudumia wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu, Lei jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za St. Mary's wakiwa wameambatana na uongozi wa shule hizo na walimu wakiweka maua katika kaburi la muasisi wa shule hizo marehemu Dkt. Getrude Rwakatare mara baada ya kumalizika kwa ibada ya shukrani, wanafunzi hao wamemwelezea Dkt. Rwakatare kama mbeba maono aliyebeba ndoto za watu wengi, leo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule za St. Mary's wakiwa katika ibada ya shukrani.

Mmoja ya wakurugenzi wa shule za St. Mary's Mutta Rwakatare akitoa neno la shukrani wa waumini wa kanisa hilo kwa maombi na sala wanazoweka kwa watoto hao na kuwaomba waendelee kuwaweka katika maombi ili wafanikiwe zaidi, Leo jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

WANAFUNZI wa shule za St. Mary's nchini wakiongozwa na wa uongozi wa shule hizo leo Januari 24 wameshiriki ibada maalumu ya shukrani kutokana na ufaulu wa juu wa shule hizo katika mitihani ya kitaifa, ibada iliyofanyika  katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Jijini Dar es Salaam. huku wanafunzi na walimu wakimwelezea muasisi wa shule hizo marehemu Askofu. Getrude Rwakatare kuwa mbeba maono yanayoendelea kuishi na kuwanufaisha wanajamii wengi.

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo Mkurugenzi wa shule hizo Dkt. Rose Rwakatare amesema, Shule hizo zimeendelea kufanya vizuri katika mitihani yao licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali.

''Tumepitia katika kipindi kigumu lakini ndoto za mbemba maono Mama Rwakatare zitaendelezwa, ametuachia watangulizi wazuri, shule zetu zina walimu waadilifu na wenye kujitoa kila leo katika kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora na yenye tija kwao na jamii kwa ujumla.'' Amesema.

Amesema kuwa katika matokeo ya mitihani katika ngazi mbalimbali yaliyotangazwa hivi karibuni shule za St. Mary's zimeendelea kufanya vizuri na kuendelea kujenga imani kwa jamii.

''Matokeo ya mtihani ya darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni shule zetu zimeendelea kufanya vizuri licha ya kupata changamoto mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona tunawashukuru walimu wetu kwa kutochoka...wanapambana katika kupeleka mbele gurudumu la elimu.'' Amesema.

Aidha amesema, Shule za msingi, Sekondari zilizopo Dar es Salaam na katika Mikoa ya Mbya, Dodoma na Morogoro pamoja na Chuo cha Ualimu bado wanaendelea kupokea wanafunzi wa ngazi zote na ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha elimu inafika kote nchini.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hizo wameushukuru uongozi wa shule hizo kwa kuendelea kuhakikisha wanapata elimu bora zaidi huku wakimwelezea muasisi wa shule hizo marehemu Dkt. Getrude Rwakatare kuwa nguzo muhimu na kiongozi aliyewaachia walimu waadilifu, wacha Mungu na wenye kujitoa kwa wanafunzi wao.

Katika misa hiyo wanafunzi kutoka shule za St. Mary's Tabata, Mbagala na Mbezi walipata nafasi ya kusali na kuweka maua katika kaburi la muasisi wa shule hizo Mama Getrude Rwakatare.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...