Picha ya pamoja ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na yaliyohusu Afya ya Uzazi kwa vijana yaliyofanyika jijini Arusha.
Waziri Njau ni Mratibu wa mkoa wa shirika hilo ,amesema kuwa jamii haswa vijana bado hawana uelewa mkubwa juu ya Afya ya uzazi,hivyo vijana wana changamoto kubwa,kwani huduma Rafiki kwa vijana hao bado haijaeleweka katika jamii
Amesema vijana wengi wanamatatizo ya Afya ya akili ,dawa za kulevya,matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango ni yapo chini kwa vijana wale ambao wameshapata ujauzito,hivyo wameomba vyombo vya habari viweze kutumika vyema ili vijana waweze kupata habari.
Dkt.Charles Migunga ni Mratibu wa Afya ya Akili katika ngazi ya mkoa amesema kuwa, vijana wengi wamekuwa wakijiingiza kwenye mambo yasiyofaa kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha ,hivyo waandishi wa habari wanapaswa kupaza sauti ili kuwanasua kutoka katika matendo hayo ,kama utumiaji wa dawa za kulevya, pamoja na kuwahabarisha kuhusu elimu ya Uzazi.
Dkt.Migunga amesema kuwa hadi sasa wameweza kuzunguka katika halmashauri ya jiji Arusha,Meru,na Arusha Dc katika shu le kadhaa za sekondari na msingi ambapo vijana kuanzia darasa la 5,6 na darasa la 7 wachache baadhi yao wameshaanza kutumia bangi,pombe mirungi, ugoro na wengine wanatumia gundi
Migunga aliongeza kuwa hali kwa jiji la Arusha siyo nzuri sana kwa vijana hao wa shule za msingi na sekondari,hivyo wamechukua jukumu la kuwaelimisha waalimu wa Afya,kwa kuwapatia masomo na mada ili waweze kufundisha.
Kwa upande wake Mratibu wa mkoa wa Arusha Afya ya mama na mtoto Belinda Mumbuli alisema kuwa Afya ya uzazi ina mapana yake, pia uzazi wa mpango ukiwemo ndani yake,hivyo changamoto nyingi wananzokutana nazo wasichana wakiwemo shuleni, ni kupoteza mwelekeo wa elimu kwani akipata ujauzito akiwa shuleni anafukuzwa.
''Anapopata mimba siyo wazazi wote wapo tayari kuishi nae nyumbani ,bali wengine watasababisha msichana huyu kuolewa katika umri mdogo hajui hili wala lile, mwisho wa siku anapata madhara maungo yake hayajakomaa,wakati wa kujifungua anapata shida wengine wanaambiwa wakazalie kwa wakunga wa jadi' inatokea shida ya kupoteza maisha aidha mama au mtoto ama tunawapoteza wote''Alisema Belinda.
Amesema changamoto nyingine kubwa wanayopitia wasichana ni kutengwa,pamoja na mtoto kukosa mahitaji muhimu,ama wakati mwingine kwa vile amepata ujauzito na hataki wazazi wafahamu anaichokonoa ,jambo amabalo linampelekea kupata matatizo, hivyo amewaomba waandishi wa habari kushirikiana kwa pamoja ili kuwaokoa vijana katika changamoto ambazo zinazowakumba juu ya Afya ya uzazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...