Moja ya tanki kati ya matanki mawili yanayojengwa kwenye mradi wa maji Madaba.Tanki hili ambalo tayari limejazwa maji na limeanza kutumika lipo katika kijiji cha Kipingo.

Moja ya matanki ambayo yanajengwa kwenye mradi wa maji Madaba katika mradi unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.31
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles akizungumzia mradi wa maji unaotekelezwa katika vijiji vinne  Madaba katika kijiji cha Kipingo.
Jumjuiya ya watumiaji maji kutoka vijiji vinne vya Mtepa,Kipingo,Lituta na Madaba Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

MRADI wa maji unaotekelezwa katika vijiji vinne vya Mtepa,Kipingo,LItuta na Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 na tayari wananchi wa kijiji cha Kipingo wameanza kupata maji.

Meneja wa Mamlaka ya Maji vijijini RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles amesema mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.3  ambapo matanki mawili yamejengwa,huku tanki moja la Kipingo limejazwa maji kwa ajili ya kuanza kuhudumia wananchi.

Hata hivyo amesema ili kukamilisha tanki moja la Madaba pachani zinasubiriwa pampu za kusukumia maji ambazo zitafungwa wakati wowote kuanzia sasa na kwamba mradi huo ni mkubwa  umehusisha ujenzi wa matanki mawili na ulazaji wa mabomba kilometa 34.

“Wananchi wa kipingo wameanza kupata maji,tunatarajia maeneo mengine yaliyobakia kati ya Januari 18 hadi 25 mwaka huu,wananchi wataanza kupata huduma ya maji,tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa kutupatia fedha zilizotekeleza mradi huu hivyo kuondoa kero ya maji kwa wananchi’’,alisema Charles.

Olaph Pilli ni Diwani wa Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba,amesema kabla ya kutekeleza mradi huu,Madaba ilikuwa na changamoto kubwa ya maji ambapo amesema mradi huu wa maji umekuwa mkombozi mkubwa katika kata yake.

“Hali ya maji katika Halmashauri yetu ya Madaba hasa katika Kata ya Lituta ilikuwa ni tete,wananchi walikuwa wanapata shida ya maji,lakini baada ya mradi huu sasa Madaba haitakuwa na shida tena ya maji,tuna maji ya kutosha’’,alisisitiza Diwani Pilli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji maji vijiji vinne vya Mtepa,Kipingo,Lituta na Madaba Modestus Mgina ameipongeza RUWASA kwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo ambapo tayari tanki moja la Kipingo limejazwa maji tayari kwa kuanza kusambazwa kwa wananchi.

Amesema mradi huo unakwenda kuwanufaisha wananchi zaidi ya 19,000 ambapo ameitaja hali ya maji kabla ya kutekeleza mradi huu ilikuwa ni mbaya,wananchi walikuwa wanapata maji ya mgawo kati ya siku tatu hadi tano.

“Maji yalikuwa yanapatikana kwa vurugu na ugomvi mkubwa,ilikuwa ni vita ya maji,lakini sasa mradi huu unamaliza kero hiyo,tunamshukuru sana Rais Dkt.John Magufuli,tuna raha sana kupata mradi huu’’,,alisema.

Desderia Ngatunga ni Mkazi wa Madaba akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Madaba, amesema wanaishukuru serikali kwa kuwapatia mradi mkubwa wa maji ambapo sasa Madaba itaneemeka kwa maji mengi ya kutosha na kumaliza kilio cha maji cha miaka mingi.Wakazi wa Madaba waanza kunufaika na mradi wa maji wa bilioni 1.3

MRADI wa maji unaotekelezwa katika vijiji vinne vya Mtepa,Kipingo,LItuta na Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 na tayari wananchi wa kijiji cha Kipingo wameanza kupata maji.

Meneja wa Mamlaka ya Maji vijijini RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles amesema mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.3  ambapo matanki mawili yamejengwa,huku tanki moja la Kipingo limejazwa maji kwa ajili ya kuanza kuhudumia wananchi.

Hata hivyo amesema ili kukamilisha tanki moja la Madaba pachani zinasubiriwa pampu za kusukumia maji ambazo zitafungwa wakati wowote kuanzia sasa na kwamba mradi huo ni mkubwa  umehusisha ujenzi wa matanki mawili na ulazaji wa mabomba kilometa 34.

“Wananchi wa kipingo wameanza kupata maji,tunatarajia maeneo mengine yaliyobakia kati ya Januari 18 hadi 25 mwaka huu,wananchi wataanza kupata huduma ya maji,tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa kutupatia fedha zilizotekeleza mradi huu hivyo kuondoa kero ya maji kwa wananchi’’,alisema Charles.

Olaph Pilli ni Diwani wa Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba,amesema kabla ya kutekeleza mradi huu,Madaba ilikuwa na changamoto kubwa ya maji ambapo amesema mradi huu wa maji umekuwa mkombozi mkubwa katika kata yake.

“Hali ya maji katika Halmashauri yetu ya Madaba hasa katika Kata ya Lituta ilikuwa ni tete,wananchi walikuwa wanapata shida ya maji,lakini baada ya mradi huu sasa Madaba haitakuwa na shida tena ya maji,tuna maji ya kutosha’’,alisisitiza Diwani Pilli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji maji vijiji vinne vya Mtepa,Kipingo,Lituta na Madaba Modestus Mgina ameipongeza RUWASA kwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo ambapo tayari tanki moja la Kipingo limejazwa maji tayari kwa kuanza kusambazwa kwa wananchi.

Amesema mradi huo unakwenda kuwanufaisha wananchi zaidi ya 19,000 ambapo ameitaja hali ya maji kabla ya kutekeleza mradi huu ilikuwa ni mbaya,wananchi walikuwa wanapata maji ya mgawo kati ya siku tatu hadi tano.

“Maji yalikuwa yanapatikana kwa vurugu na ugomvi mkubwa,ilikuwa ni vita ya maji,lakini sasa mradi huu unamaliza kero hiyo,tunamshukuru sana Rais Dkt.John Magufuli,tuna raha sana kupata mradi huu’’,,alisema.

Desderia Ngatunga ni Mkazi wa Madaba akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Madaba, amesema wanaishukuru serikali kwa kuwapatia mradi mkubwa wa maji ambapo sasa Madaba itaneemeka kwa maji mengi ya kutosha na kumaliza kilio cha maji cha miaka mingi.

Na Albano Midelo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...