Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Catherine Kameka akiwahudumia wananchi waliofika katika Banda la NHIF kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Afisa Matekelezo wa NHIF Amandus Machal akiwapa maelezo kuhusiana Mfuko unavyofanya kazi katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Baadhi ya wananchi wakipata taarifa ya Elimu ya  Mfuko huo  katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Afisa Matekelezo wa NHF Sunday Matoi akimhudumia baadhi ya wananchi wakipata taarifa ya Elimu ya  Mfuko huo  katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma


*NHIF yaahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi 

Na Ripota Wetu, Michuzi Tv

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema kuwa katika kulinda afya ni kuwa na Bima ya Afya ambayo itafanya kuwa na uhakika wa matibabu bila ya kuwa na fedha.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma  Afisa Uhusiano wa NHIF Catherine Kameka amesema wananchi watumie fursa ya maadhimisho hayo kupata elimu na mrejesho wa taarifa mbalimbali kuhusu Mfuko.

Amesema kuwa Mfuko uko kwa ajili ya kuwahudumia watanzania ili kuwa na uhakika wa matibabu.

Aidha amesema kuna aina mbalimbali za kujiunga na Mfuko kutokana na mtu anavyohitaji na vyote vinafanya kazi.

Kameka amesema kuwa mwitikio ni mkubwa kwa wananchi kujiunga na Mfuko na kupata elimu namna Mfuko unavyofanya kazi.

Amesema Serikali nia yake ni kuona wananchi wake hawapati changamoto za matibabu ndio maana ikaweka mfuko huo huku Serikali ya awamu ya Tano inayokwenda kasi katika uchumi ikitaka kulinda rasilimali watu yenye afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...