Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro (MB) akihutubia wakazi wa Songea kwenye Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 114 ya Vita vya Maji Maji na Tamasha la Utalii na Utamaduni, Songea Mkoa wa Ruvuma

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro (MB) alipo katikati, akipokea malezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel  Lwoga (Wapili kulia) kwenye Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 114 ya Vita vya Maji Maji na Tamasha la Utalii na Utamaduni, Songea Mkoa wa Ruvuma

Klabu ya Historia ambao ni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mfaranyaki wakiigiza kichocheo cha Vita ya Maji Maji, kwenye Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 114 ya Vita vya Maji Maji na Tamasha la Utalii na Utamaduni, Songea Mkoa wa Ruvuma

Klabu ya Historia ambao ni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Matogoro wakicheza Ngoma ya Mganda katika kuuenzi Utamaduni,  kwenye Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 114 ya Vita vya Maji Maji na Tamasha la Utalii na Utamaduni, Songea Mkoa wa Ruvuma.

**************************************

Na Sixmund J. Begashe

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa imetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli la kufundisha historia ya kitanzania mashuleni na kwenye vyuo mbali mbali nchini, kwa kuanzisha Klabu za Historia na Uzalendo mashuleni na kuzilea kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu na Utamaduni.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro alipofungua rasmi Maadhimisho  ya Kumbukizi ya Miaka 114 ya Vita vya Maji Maji na Tamasha la Utalii na Utamaduni wa makabila ya Mkoa wa Ruvuma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Makumbusho ya Maji Maji Songea Mkoani Ruvuma.

Dkt Ndumbaro amesisitiza kuwa Wizara yake itaendelea kuwaenzi Mashujaa wa Vita vya Maji Maji na wote walio jitoa kwa taifa letu kwa kuboresha Maeneo ya Kihistoria na kutoa elimu kupitia Makongamano na Matamasha ili jamii hasa kizazi cha sasa kiweze kurithi uzalendo wa wazee wetu.

“Niwaahidi kuwa Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa Mkoa wa Ruvuma kwa kuhakikisha kuwa tamasha hili linaendelea kufanyika kwani pia ni utekelezaji wa Ibara ya 71 (h) ya Ilani ya CCM 2020-2025 ambayo imeweka bayana ushirikishwaji wa jamii katika kufanya matamasha ya kitamaduni na kuyatumia kutangaza na kukuza utalii wa malikale na utamaduni” Alisema Dkt Ndumbaro

Akimkaribisha Mgeni rasmi kwa niaba ya katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Christowaja Ntandu (Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mambo Kale) ameeleza kuwa katika kutekeleza shughuli mbali mbali za uhifadhi wa Urithi wa Asili na Utamaduni Wizara imeweka mikakati ya kuimarisha Shirika la Makumbusho ya Taifa ili liweze kusimamia ipasavyo utafiti, uhifadhi na uendeshaji wa sekta ya Malikale kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.

Akielezea sababu za kuwa na programu ya klabu za Historia mashuleni, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noeli Lwoga amesema ni kukuza ufahamu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kuhusu Historia ya Tanzania, juhudi za wazee wetu katika kuleta ukombozi na kukuza uzalendo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Makumbusho ya Taifa Sura 281, Makumbusho ya Taifa la Tanzania ni Taasisi ya Kielimu na Kiutamaduni yenye jukumu la kukusanya, kutafiti, kuhifadhi na kuelimisha jamii kuhusu urithi wa Taifa. Hivyo, ina wajibu wa kutoa mchango wake katika kufundisha historia ya Tanzania kwa vitendo, na hivyo kutekeleza Agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli” Aliongeza Dkt Lwoga

Klabu za historia Mashuleni zimezinduliwa katika shule za Sekondari  Bombambili, Mashujaa, Matogoro, De Paul, Mfaranyaki na Skillpath zote za mjini Songea ambapo wanafunzi wa shule hizo walipata kuonesha umahiri wao wa kuelezea historia ya viongozi mbali mbali na historia ya Vita vya Maji maji vilivyo piganwa  kwa miaka miwili 1905 hadi 1907.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...