Charles James, Michuzi TV

SHIRIKA la Chakula na Kilimo Ulimwenuni (FAO) limesema linaamini kwa kushirikiana uliopo baina yao na Serikali ya Tanzania watafanikisha malengo yao ya kumaliza changamoto za uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma pamoja na kuboresha miundombinu ya ufanyaji kazi wa sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Mtaalamu wa Uvuvi kutoka Shirika la FAO, Hashim Muumini wakati akizungumza na wandishi wa habari mkoani Kigoma baada ya kutembelea na kujionea shughuli za uvuvi zinazofanywa kwenye Ziwa Tanganyika.

Muumin amesema FAO kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Uvuvi na Mifugo chini ya Taasisi yake ya Uvuvi ya TAFIRI wamekusudia changamoto ya wadau wote wa Ziwa Tanganyika kuanzia Wavuvi, Wasafirishaji wa mazao ya uvuvi nje ya nchi, wafanyabiashara hadi wanunuzi.

Amesema kupitia mradi wa FISH4ACP ambao utatekelezwa kwenye Nchi 12 ukifadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Ujerumani unagharimu kiasi cha Euro Milioni 40 huku Tanzania ikinufaika pia na mradi huo kwa kutengewa kiasi cha Euro Milioni Tatu.

" Sisi kama FAO tunaishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Utafiti ya TAFIRI ambapo kwenye mradi huu tumepanga kwanza kujua changamoto zinazowakabili wadau wa uvuvi na kuja na mikakati ya kufungua fursa za Ziwa Tanganyika na baada ya hapo ndio tutaanza kuyatatua matatizo yao. 

Tumelenga kugusa changamoto zao kuanzia kwenye Masoko ya ndani na nje ya nchi, uchakataji samaki, nyavu au hata kama kuna matatizo mengine watatueleza na lengo letu ni kuirasimisha sekta hii ya uvuvi hapa Ziwa Tanganyika.

Amesema mradi wa FISH4ACP utaanza kuangazia changamoto hizo kuanzia mwezi Machi mwaka huu ambapo wamepanga kuwatembelea wadau wote wa Ziwa Tanganyika kujua changamoto zao ili kuangalia namna gani wanaweza kutengeneza mikakati ya kuitatua.

" Huu ni mradi wa miaka mitano ambapo malengo yetu ni kuondoa changamoto zote kuanzia kwa wavuvi wale wanaovua samaki hadi kwa walaji kwenye sahani, tunaamini miaka mitano tutakua tunazungumzia mafanikio makubwa ya Ziwa Tanganyika yaliyoletwa na mradi huu wa FISH4ACP, tunaomba wavuvi na wadau wote wawe wavumilivu na tunapowafikia watueleze bila kuficha changamoto zao ili tuzijue na kuzifanyia kazi, sisi FAO tuna mafanikio makubwa sana kwenye kufanya mapinduzi ya uvuvi, tunaamini na hapa tutaweka historia," Amesema Muumin.

Baadhi ya wavuvi wa Ziwa Tanganyika wakirudi asubuhi kutokea Ziwani walipoenda kuvua samaki usiku.
Baadhi ya wavuvi wa Ziwa Tanganyika wakirudi asubuhi kutokea Ziwani walipoenda kuvua samaki usiku.
Hii ni Alfajiri ambapo wavuvi wa Ziwa Tanganyika wakiwa wanarejea nchi kavu wakitokea ziwani ambapo kwa usiku mzima walikua wakifanya biashara zao za uvuvi.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...