Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-Arusha

   
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha  mkoani Arusha  limepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 yenye makisio yenye thamani ya sh.57,164,979,345.36 bilioni.

 Mpango huo umepitishwa leo Febuari,25 ,mwaka 2021 wilayani Arumeru na Madiwani wa Halmashauri ya Arusha  katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
  
 Akizungumza  Katika baraza hili maalum la  Madiwani ,  Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Saad Mtambule, alisema katika rasimu hiyo fedha za miradi ya maendeleo ni sh. 10,264,014,705.36 na fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ni sh.4,422,748,752,00
 
 Alisema mpango huo  umezingatia kanuni zote hivyo madiwani wameupitisha kwa malengo ya afya ya maendeneo ya Halmashauri, upande wa mishahara Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia jumla ya sh.40,897,610,000.00na kwa upande wa  matumizi mengineyo ni sh.1,580,605,888.00
  
 Aidha aliongeza kuwa watahakikisha wanatoa huduma bora itakayo saidia kuongeza ukusanyaji wa mapato Ili kuweza kufikia lengo kwa asilimia  100.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Ojung'u Salekwa, akifungua mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa kujadili na kupitisha Mpango wa bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2021/2022, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha , alisema kuwa katika mpango wa Bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2021/2022, halmashauri imeweka kipaumbele katika kuboresha mbinu za ukusanyaji wa mapato ya Ndani ili kuweza kutataua changamoto zinazokabili halamshauri kisekta kwa miundombinu kakta ya Elimu, Afya, maji, umeme, miundombinu ya bararaba, pamoja maendeleo ya Jamii kwa ujumla wake.

Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hilo la Madiwani kuipitia na kuichambua bajeti hiyo sambamba na vipaumbele vyake, lengo likiwa ni kuborehsa huduma za jamii kwa wananchi wa halmashauri ya Arusha na kuifanya Jamii kuwa na Maendeleo endlelevu katika sekta zote.

Aidha aliwataka madiwani kutoa taarifa kwa serikalini wanapoona dalili zozote za nzige Katika maeneo yao ,huku akiwasisitiza waendelee kuchukuwa taathari juu ya ugonjwa huu wa kushindwa kupumua pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi bila kusahau kumuomba Mungu aondoe janga hili.

  Diwani wa kata Olorien  Erick Semboja  alisema anaipongeza rasimu hiyo ya bajeti na kwamba imezingatia vipaumbele vya Halmashauri hiyo na kwamba wao kama madiwani watahakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa nguvu zote ili kufanikisha bajeti hiyo.

Alisema bajeti hiyo ni nzuri kwakuwa itamgusa mwananchi mmoja mmoja ,pia Katika bajeti hii wameangalia vipaumbele Kama barabara ,elimu na hata Katika eneo la afya.
  
 Aliwataka madiwani kutoa taarifa pindi serikalini wanapoona dalili zozote za nzige Katika maeneo yao ,huku akiwasisitiza waendelee kuchukuwa taathari juu ya ugonjwa huu wa kushindwa kupumua pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi bila kusahau kumuomba Mungu aondoe janga hili
Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Saad Mtambule akiongea Katika Kikao maalum Cha madiwani kilichofanyika Katika ukumbi wa halimashauri huyo.    
Madiwani wa halmashauri ya Arusha wakifuatilia Kikao hicho.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...