Na Said Mwishehe, Michuzi TV 


TAASISI ya Can Tanzania ambayo imejikita katika utunzaji wa mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi imewakutanisha wanachama wake katika Mkutano Mkuu wa mwaka na kufikia makubaliano kadhaa yakiwemo ya kuanza kulipa ada.

Wakati wa mkutano huo mkuu wa mwaka, Can Tanzania kupitia wanachama wake wamezungumza kwa kina kuhusu mafanikio ambayo wameyafikia na kuweka malengo ya kwenda mbali zaidi ikiwa pamoja na wanachama kuanza kujengewa uwezo kupitia wao wenyewe kwani wanao wasomi na watu wenye weledi wa kutosha.

Akizungumza na Michuzi TV baada ya kufanyika kwa mkutano huo ambao umefanyika kwa siku mbili Bunju B jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Can Tanzania Dk.Sixbert .Mwanga amesema kwenye mkutano huo umewakutanisha wanachama wao kutoka mikoa mbalimbali nchini na wamejadiliana mambo mengi.

"Tulianza kikao kwa kujadili ugonjwa Covid unavyoathiri shughuli zetu na hasa upande wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi inavyoongeza mzigo kwa wale watu wadogo wadogo kama wakulima, wafugaji, wavuvi ambao tayari walishakuwa wameathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

"Hivi sasa Corona imeongeza athari zaidi, hivyo tumeangalia namna gani tunaweza kupata fedha, tukashawishi nchi zilizoendelea na Serakali zetu pia ili kuwa na sera imara ambazo zinaangalia mbele zaidi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi , katika hali yoyote bila kujali kuna Corona au hakuna Corona,"amesema Dk.Mwanga.

Aidha wamejadili namna mtandao wao unaaweza kuwapa sauti wanachama wao wakaja pamoja kwa ajili ya kutoa mchango mkubwa katika mtandao wao kukua, kuleta majibu chanya katika kutatua changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi. 


"Lakini kingine ilikuwa ni kuangalia kwa jinsi gani mtandao unaweza kujiendesha bila kutegemea wafadhili walioko nchini, hivyo ndivyo ambavyo tumeviangalia kwa mapana kupitia Mkutano Mkuu wa mwaka,"amesema.

Akizungumzia mikakati iliyowekwa katika mkutano huo mkuu wa mwaka ambao umekuwa wenye mafanikio makubwa, Dk.Mwanga amesema  cha kwanza wamekukubaliana wanachama wao kuanza kulipa ada ya uanachama.

"Tumeweka mikakati mingi lakini la kwanza ni kuhakikisha wanachama wanaanza kulipa ada, zamani ilikuwa ili uwaite wanachama lazima uanze kutafuta fedha halafu uwaite lakini sasa wanaona faida za mtandao wetu na kwa kauli moja wamekubalia kuanza kuchangia na tutaanza mwaka huu.

"Mkakati wa pili ambao tumeafikiana ni kuanza kujengena uwezo sisi wenyewe ikiwa pamoja na kufafuta rasirimali kwasababu tunayo timu ya kutosha na mkakati wa tatu tumekubaliana sasa kuongeza kasi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

"Ikiwa pamoja na kuhakikisha tunaongeza sauti za watu walioko chini na kuzileta kwenye mtandao na kisha kuzichukua sauti hizo kupeleka kwenye ngazi za kimaifa, kwa mfano tunatarajia kuwa na mkutano unaotarajia kufanyika Novemba mwaka huu nchini Uingereza iwapo hakutakuwa na Corona,"amesema Dk.Mwanga.

Ameongeza kwamba wamekubaliana kuendelea na mikutano mingine ya wanachama pamoja na kuendelea na miradi mingine ambayo wanatakiwa kuitekeleza kwa kauli moja.

Alipoulizwa iwapo taasisi hiyo inapiga hatua au imedumaa, Dk.Mwanga amejibu wamepiga hatua kubwa ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye ni yeye."Hivi sasa taasisi imekuwa kubwa sana , idadi ya watu walioko tu ofisini imefikia 13 na kati ya hao hatujaweka wale wa kimataifa ambao wanafanya kazi kwenye taasisi yetu.

"Ni mkweli kabisa hata kwenye kutafuta rasilimali na vitendo kazi tumeimarika sana,ingawa nafikiri tunayo changamoto kule kwa wanachama wetu ni kama kumedumaa kidogo , kwasababu wengine walikuwa wanashindwa kuendana na matakwa ya Msajili wa taasisi zisizokuwa za kiserikali kwa hiyo wengine walifutwa.

"Hata hivyo hatuna shida ya kuwa 200 bali tunatoa mchango gani kwa hao 10 tuliona na wao wanatoa mchango gani kwa wale wanafanya nao kazi kule chini lakini tofauti na hapo miradi imeongezeka, tunatekeleza miradi mingi na uwezo wa kufanya kazi na Serikali na kutoa mchango unaoeleweka nao umeongezeka.

"Tumekuwa na watu wasomi ndani ya taasisi, tunao watu wenye uelewa mkubwa wa mambo, na tumeongeza uaminifu kwani tunao uwezo wa kuleta vikao vya kimataifa vikafanyika hapa nchini kama tulivyofanya mwaka 2020 jijini Arusha,"amesema.

Ameongeza  pia wamepata nafasi ya kuwa watu ambao watasajili na kuichukua Can Afrika kuileta hapa kama sekretarieti."Kwa hiyo naweza kueleza Can Tanzania imekuwa sana na  sio tu nchini bali hata Bara la Afrika linajua tunakwenda spidi.

"Na ndio maana katika mashindano hayo ambapo tulikuwa na nchi ya Afrika Kusini, Rwanda na Kenya tuliweza kushinda kwasababu ya vitu ambavyo tunafanya vinaonekana na kila mmoja wetu,"amesema Dk.Mwanga.

01:Mkurugenzi Mkuu wa Can Tanzania Dk.Sixbert Mwanga(wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa Mkutano Muu wa taasisi hiyo uliwaokutanisha wanachama wao wake kutoka mikoa mbalimbali nchini.Wengine ni wajumbe wa bodi na wawakilishi.
Dk.Sixbert Mwanga ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Can Tanzania akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Bunju B jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa taasisi hiyo wakiwa katika Mkutano Mkuu wa mwaka wakiendelea na majadiliano mbalimbali yaliyokuwa yamelenga kuweka mikakati ya kuhakikisha wanaendelea kutekeleza majukumu yako.
Meneja Miradi wa S MEC Fund-Same Bernard Wilfred akitoa maoni yake wakati wa mkutano huo.

 Ofisa Miradi kutoka Can Tanzania Jophillene Bajumula akitoa mada kwa wanachama waliohudhuria mkutano mkuu uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

 


Ofisa Miradi kutoka Can Tanzania Jophillene Bajumula akitoa mada kwa wanachama waliohudhuria mkutano mkuu uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Programu Can Tanzania Boniveture Mchomvu akizungumza mbele ya wanachama wakati wa mkutano mkuu wa mwaka.
Meneja Miradi kutoka Pelum Tanzania-Morogoro Rehema Fidelis akitoa maelezo kwa wanachama wa Can Tanzania wakati wa mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...