Waziri wa Nishati DkMedrad Kelemani (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (kushoto) na Mtendaji Mkuu TANESCO DK.Tito Mwinuka(kulia) wakiwa kwenye mkutano wa kikao kazi kilichowahusisha wahariri kabla ya kufanyika kwa uzinduzi rasmi .
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare akifuatilia jambo wakati wa kikao kazi kati ya maofisa waandamizi wa TANESCO na wahariri ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nishati Dk.Medrard Kalemani.

Matukio katika picha wakati wa kikao hicho kikiendelea baada ya kufunguliwa rasmi.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Morogoro

MKUU wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare amesema Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) limekuwa likifanya kazi kubwa ndani ya mkoa huo na vijiji ambavyo havina umeme hadi sasa ni 14 tu na tayari mpango mkakati wa kuhakikisha vinawekwa umeme.

Amesema hayo leo mbele ya Waziri wa Nishati Dk.Medrard Kalemani, maofisa waandamzi wa TANESCO wakiongozwa na Mtendaji wao Mkuu wa TANESCO Dk.Tito Mwinuka pamoja na wahariri waandamizi wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani Morogoro.

Loata Sanare amesema kwa niaba ya wenzake Mkoa wa Morogoro wanaishukuru TANESCO  kwa kuendelea kushirikiana nao wakati wote, pale kwenye changamoto wanapata ufumbuzi na kubwa zaidi wamekuwa wakipata ushirikiano wa kutosha.

"Kupitia mradi wa REA umeme umetapataa katika mkoa mzima, ni vijiji 14 tu ndio bado havipata umeme lakini umewekwa utaratibu na vyote vitapata,"amesema na kuongeza mkoa huo unajivunia kuwa sehemu yenye vyanzo vingi vya vinavyotumika kuzalisha umeme .

Amefafanua katika mkoa huo kuna Kidato inayozalisha megawati 200, Kihans inazalisha megawati 160 na sasa kuna mradi mkubwa wa Julius Nyerere ambao unaendelea na utakapokamilika utazalisha megawati 2115.

"Hivyo ukichukua mradi wa Bwawa la Julius Nyerere pamoja na vyanzo vingine mkoa wetu wa Morogoro utakuwa unazalisha zadi ya megawati 2475.Itakuwa nusu ya umeme unalozalishwa nchini unatoka kwetu.

"Hiyo itakuwa heshima kubwa kwa Mkoa wa Morogoro na ndio maana tunaendelea kuhakikisha tunalinda vyanzo vyote vya maji.Mradi wa Julius Nyerere utakapokamilika manufaa yake hayatakuwa kwa Mkoa huu tu au kwa nchi peke bali pamoja na nchi jirani ambazo zinatuzunguka.

"Tunamshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa maoni yake makubwa ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa.Tunashuhudia kazi kubwa inayofanyika kwenye mradi huo, tunajua Rais ataondoka lakini atakuwa ameacha alama kubwa katika nchi yetu,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...